title : DIT YABUNI MASHINE MAALUM YA KUTENGENEZA MKAA MBADALA, YAWA KIVUTIO MAONESHO WIKI YA MAZINGIRA
kiungo : DIT YABUNI MASHINE MAALUM YA KUTENGENEZA MKAA MBADALA, YAWA KIVUTIO MAONESHO WIKI YA MAZINGIRA
DIT YABUNI MASHINE MAALUM YA KUTENGENEZA MKAA MBADALA, YAWA KIVUTIO MAONESHO WIKI YA MAZINGIRA
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
TAASISI ya Teknolojia ya Dar es Salaam(DIT), imeamua kubuni na kuzindua mashine maalumu ya kutengenezea mkaa mbadala.
Lengo la kubuni mashine hiyo ni jitihada za DIT katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kupitia mikakati yake ya kukabiliana na uharibufu wa misitu na utunzaji wa mazingira.
Akizungumzia kuhusu umuhim wa mashine hiyo leo kwenye Maonyesho ya Wiki ya Mazingira yanayoyendelea Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Mkufunzi wa Idara ya Uhandisi wa Mitambo wa taasisi hiyo Asaph Kagina, amefafanua mashine hiyo yenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya tani tatu za mkaa kwa siku ni suluhisho tosha katika kulinda misitu hapa nchini.
Amesema kuwa mashine hiyo inayotumia mabaki ya mazao mashambani, zikiwemo pumba za mpunga, mahindi, vifuu vya nazi, pumba pamoja na makaa ya mawe, imeundwa kutokana na wazo lilitokana na ripoti maalumu ya Banki ya Dunia kuhusu hali ya mazingira, pamoja na ripoti nyingine ya aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Misitu na nyuki Dk. Felician Kilahama.

Mkufunzi wa Idara ya Uhandisi wa Mitambo kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam(DIT)akifafanua jambo kwa baadhi waandishi waliotaka kufahamu kwa kina machine ya kuzalisha mkaa mbadala ambayo imebuniwa na taasisi hiyo
Mkufunzi wa Idara ya Uhandisi Mitambo Katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam(DIT) Akita maelezo ya machine maalum ambayo imebuniwa na taasisi hiyo ambayo inazalisha mkaa mbadala
Mashine ya kutengeneza mkaa mbadala ambayo imebuniwa na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT).
Hivyo makala DIT YABUNI MASHINE MAALUM YA KUTENGENEZA MKAA MBADALA, YAWA KIVUTIO MAONESHO WIKI YA MAZINGIRA
yaani makala yote DIT YABUNI MASHINE MAALUM YA KUTENGENEZA MKAA MBADALA, YAWA KIVUTIO MAONESHO WIKI YA MAZINGIRA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DIT YABUNI MASHINE MAALUM YA KUTENGENEZA MKAA MBADALA, YAWA KIVUTIO MAONESHO WIKI YA MAZINGIRA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/dit-yabuni-mashine-maalum-ya.html
0 Response to "DIT YABUNI MASHINE MAALUM YA KUTENGENEZA MKAA MBADALA, YAWA KIVUTIO MAONESHO WIKI YA MAZINGIRA"
Post a Comment