WIZARA YA AFYA YAMWAGA AJIRA 8,000 SEKTA YA AFYA NCHINI

WIZARA YA AFYA YAMWAGA AJIRA 8,000 SEKTA YA AFYA NCHINI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WIZARA YA AFYA YAMWAGA AJIRA 8,000 SEKTA YA AFYA NCHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WIZARA YA AFYA YAMWAGA AJIRA 8,000 SEKTA YA AFYA NCHINI
kiungo : WIZARA YA AFYA YAMWAGA AJIRA 8,000 SEKTA YA AFYA NCHINI

soma pia


WIZARA YA AFYA YAMWAGA AJIRA 8,000 SEKTA YA AFYA NCHINI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
                                                                                            
  Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepata kibali cha Ajira kwa sekta ya afya nchini cha kuwaajiri wataalam wa kada mbalimbali za Afya wapatao 8,000.

Hayo ya mesemwa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya.

Dkt. Mpoki amesema wamepata kibali hicho kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na kuongeza kwamba Wizara yake inalo jukumu la kuwapangia vituo vya kazi waombaji wenye sifa kwa mujibu wa waraka wa Maendeleo ya Utumishi wa Umma Namba 1 wa mwaka 2009 kuhusu miundo ya utumishi wa kada za afya chini ya Wizara ya Afya.

Aidha, alisema kibali hicho chenye aina mbili za mwajiri ikiwepo nafasi 6,180 ambazo zimeenda Hospitali zilizo katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwenye hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati. Nafasi 1,820 zimeenda Hospitali zilizo chini ya Wizara ya Afya, Hospitali za Rufaa za Mikoa, Wizara zingine na Taasisi za Umma pamoja na Hospitali ya Mlongazila na Benjamini Mkapa.

Alitaja sifa za waombaji wa nafasi hizo kuwa, awe raia wa Tanzania, umri usiozidi miaka 45, asiwe mwajiri wa Serikali au mwajiriwa wa Hospitali za Mashirika ya Dini ambaye mshahara wake unalipwa na Serikali na asiwe ameshawahi kufanya kazi Serikalini na kuacha kazi.Hata hivyo, Dkt. Mpoki amewakumbusha wataalam hasa wale wanaosajiliwa na mabaraza ya kitaaluma kuambatanisha nakala za usajili au leseni ya kufanya kazi ya taaluma husika wakati wa maombi hayo.

Katibu Mkuu ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano na kueleza kuwa nafasi hizi 8,000 ni juhudi za Serikali za kupunguza uhaba wa rasilimali watu katika sekta ya afya. 

Imetolewa na : 
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Afya 
11/5/2018


Hivyo makala WIZARA YA AFYA YAMWAGA AJIRA 8,000 SEKTA YA AFYA NCHINI

yaani makala yote WIZARA YA AFYA YAMWAGA AJIRA 8,000 SEKTA YA AFYA NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WIZARA YA AFYA YAMWAGA AJIRA 8,000 SEKTA YA AFYA NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/wizara-ya-afya-yamwaga-ajira-8000-sekta.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WIZARA YA AFYA YAMWAGA AJIRA 8,000 SEKTA YA AFYA NCHINI"

Post a Comment