title : EfG YAZINDUA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA JIJINI DAR ES SALAAM
kiungo : EfG YAZINDUA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA JIJINI DAR ES SALAAM
EfG YAZINDUA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA JIJINI DAR ES SALAAM
Na Dotto Mwaibale
SHIRIKA la Equality for Growth (EfG) lenye makao makuu yake jijini Dar es Salaam, jana limezindua siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kama taifa na kuungana na mataifa mengine duniani katika maadhimisho hayo.
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika Soko la Tabata Muslim Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa shirika hilo, Jane Magigita amesema kwa sasa EfG inaendesha mradi unaoitwa "MPE RIZIKI SI MATUSI" ambao umeongeza wigo wa mapambano ya ukatili wa kijinsia katika Wilaya ya Ilala na Temeke katika masoko sita.
Ameyataja masoko hayo kuwa ni Mchikichini, Kisutu,Tabata Muslim, Feri, Gezaulole na Temeke Stereo.
Magigita aliongeza kuwa, lengo la mradi huo ni kuona wanawake wafanyabiashara wa Manispaa ya Ilala na Temeke wanafanyabiashara katika mazingira huru dhidi ya ukatili wa kingono, kimwili, matusi na kisiasa, vilevile kuona wanawake wakipewa heshima kama binadamu wengine ili waweze kujipatia kipato chao bila vikwazo.
"Mbali na kuwepo mashirika mbalimbali yanayojihusisha na masuala ya ukatili wa kijinsia, EfG pekee ndiyo ambayo inajihusisha na kuwasaidia wafanyabiashara katika masoko na kuwapa elimu ya haki za binadamu, sheria na ukatili wa kijinsia," alisema mkurugenzi huyo na kuongeza;
Mkurugenzi wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita akihutubia katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika Dar es Salaam jana Soko la Tabata Muslim.
Mratibu wa Mradi wa Mpe Riziki Si Matusi, Susan Sita akimpatia fulana Mwakilishi wa Mbunge wa Segerea, Bonah Kaluwa aliyefika kwaniaba yake kama mgeni rasmi, Shanisudin Ahmed wakati wa uzinduzi huo.
Hivyo makala EfG YAZINDUA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA JIJINI DAR ES SALAAM
yaani makala yote EfG YAZINDUA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA JIJINI DAR ES SALAAM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala EfG YAZINDUA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA JIJINI DAR ES SALAAM mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/efg-yazindua-siku-16-za-kupinga-ukatili_2.html
0 Response to "EfG YAZINDUA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA JIJINI DAR ES SALAAM"
Post a Comment