title : NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, JAPHET HASUNGA AFUNGUA KITUO CHA MAFUNZO YA MISITU NA UCHAKATAJI WA MAGOGO MKOANI IRINGA
kiungo : NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, JAPHET HASUNGA AFUNGUA KITUO CHA MAFUNZO YA MISITU NA UCHAKATAJI WA MAGOGO MKOANI IRINGA
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, JAPHET HASUNGA AFUNGUA KITUO CHA MAFUNZO YA MISITU NA UCHAKATAJI WA MAGOGO MKOANI IRINGA
Na Hamza Temba-WMU-Iringa
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga amefungua Kituo cha Mafunzo ya Misitu na Uchakataji wa Magogo ambacho kimeanzishwa katika Mji wa Mafinga, Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa chini ya ufadhili wa Serikali ya Finland kupitia mradi wa Panda Miti Kibiashara.
Akizungumza kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa kituo hicho jana mjini hapa, Naibu Waziri Hasunga ameishukuru Serikali ya Finland kwa msaada huo na misaada mingine ambayo imekuwa ikiitoa katika kuimarisha sekta ya Misitu nchini toka miaka ya 1970s.
Alisema lengo la kituo hicho ni kusaidia kutoa elimu kwa vitendo na ujuzi kwa makundi mbalimbali ambayo yapo katika mnyororo wa kuongeza thamani ya mazao ya misitu ikiwemo watu binafsi, viwanda vya misitu na taasisi za Serikali kuanzia hatua za mwanzo za upandaji wa miche ya miti hadi kwenye hatua za mwisho za uchakataji wa magogo.
Aidha, kutokana na kituo hicho kuwa chini ya mradi huo, Naibu Waziri Hasunga amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja Jenerali Gaudence Milanzi kuangalia uwezekano wa kukiweka kituo hicho chini ya Wizara yake ili mafunzo yanayotolewa yawe endelevu hata kama mradi husika utafikia ukiongoni.Pia, ameagiza mitaala ya kituo hicho ipitiwe na isajiliwe kupitia Mfumo wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi– VETA ili yaweze kutambulika na wahitimu wapewe vyeti kulingana na mahitaji ya soko katika sekta ya viwanda vya misitu nchini.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) na Balozi wa Finland nchini, Mhe. Peka Huka wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Kituo cha Mafunzo ya Misitu na Uchakataji wa Magogo kilichoanzishwa mwezi Desemba, 2016 katika mji wa Mafinga, Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa chini ya ufadhili wa Serikali ya Finland katika hafla iliyofanyika jana mkoani humo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akipanda mti wa kumbukumbu muda mfupi baada ya kufungua rasmi Kituo cha Mafunzo ya Misitu na Uchakataji wa Magogo kilichoanzishwa katika mji wa Mafinga, Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa chini ya ufadhili wa Serikali ya Finland. Kutoka kushoto wa tatu ni Balozi wa Finland nchini, Mhe. Peka Huka, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza.
Balozi wa Finland nchini Tanzania, Mhe. Peka Huka akipanda mti wa kumbukumbu muda mfupi baada ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) kufungua rasmi Kituo cha Mafunzo ya Misitu na Uchakataji wa Magogo kilichoanzishwa mwezi Desemba, 2016 katika mji wa Mafinga, Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa chini ya ufadhili wa Serikali ya Finland. Kutoka kulia wa tatu ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Christina Mndeme na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi jana muda mfupi baada ya kufungua rasmi Kituo cha Mafunzo ya Misitu na Uchakataji wa Magogo kilichoanzishwa mwezi Desemba, 2016 katika mji wa Mafinga, Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa chini ya ufadhili wa Serikali ya Finland. Wengine pichani ni Balozi wa Finland nchini, Mhe. Peka Huka (wa pili kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Christina Mndeme.
Hivyo makala NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, JAPHET HASUNGA AFUNGUA KITUO CHA MAFUNZO YA MISITU NA UCHAKATAJI WA MAGOGO MKOANI IRINGA
yaani makala yote NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, JAPHET HASUNGA AFUNGUA KITUO CHA MAFUNZO YA MISITU NA UCHAKATAJI WA MAGOGO MKOANI IRINGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, JAPHET HASUNGA AFUNGUA KITUO CHA MAFUNZO YA MISITU NA UCHAKATAJI WA MAGOGO MKOANI IRINGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/naibu-waziri-wa-maliasili-japhet.html
0 Response to "NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, JAPHET HASUNGA AFUNGUA KITUO CHA MAFUNZO YA MISITU NA UCHAKATAJI WA MAGOGO MKOANI IRINGA"
Post a Comment