title : TBC, KWESE FREE SPORTS (TV1) KURUSHA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA (FIFA) BURE KWA KISWAHILI
kiungo : TBC, KWESE FREE SPORTS (TV1) KURUSHA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA (FIFA) BURE KWA KISWAHILI
TBC, KWESE FREE SPORTS (TV1) KURUSHA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA (FIFA) BURE KWA KISWAHILI
Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii
KITUO cha Televisheni ya Taifa (TBC), TBC Taifa na Kwese Free Sports (TV1) wameingia makubaliano ya kurusha matangazo ya moja kwa moja ya michuano ya kombe la Dunia (FIFA World cup 2018) bure kabisa kwa lugha adhimu ya Kiswahili yatakayoanza 14 Juni hadi 15 Julai mwaka huu huko Moscow Urusi.
Akizungumza katika hafla ya makubaliano hayo leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa TBC Dk.Ayoub Rioba amesema huu ni wakati wa wananchi kufurahia michuano hiyo kupitia televisheni ya taifa bure kabisa na kwa lugha ya Kiswahili.
Ameeleza kuwa watanzania wategemee mambo mazuri kupitia Kwese Free Sports wakiwa sambamba na TBC1 na TBC Taifa.Kwa upande wa Mkurugenzi wa Kwese Free Sports (TV1) Joseph Sayi amesema wameamua kuwaletea watanzania uhuru wa kufurahia bure kabisa kwa kuangalia michuano hiyo na kusikiliza kupitia TBC Taifa kwa lugha ya Kiswahili.
Meneja Masoko TBC Dafrosa Kimbory ameeleza kuwa licha ya watanzania kupata burudani hii pia ni fursa kwa wafanyabiashara kwa kutangaza bidhaa zao na wanaamini watawafikia watanzania wengi zaidi.
Aidha Mkurugenzi Kitengo cha Mawasiliano TBC amewashukuru Kwese kwa ushirikiano na kueleza kuwa hii ni fursa kwao katika kubadilishana uzoefu wa kiteknolojia na maudhui na matangazo hayo yataanza hivi punde na kuendelea hadi mashindano yatakapoisha.
Aidha Walter Kimaro mbunifu kutoka TV1 ameeleza kuwa wamejipanga na hadi sasa studio kabambe imeandaliwa kwa shughuli hiyo hivyo watanzania watarajie mambo mazuri kutoka kwao.
Akizungumza kuhusu Kwese Free Sports Mkurugenzi mtendaji wa Kwese Free Sports Mgope Kiwanga ameeleza kuwa Kwese Free Sports ilianzishwa mwaka 2014 ikijulikana kama TV1 na baadaye kuwa Kwese Free Sports na Chaneli hii imelenga kuwaburudisha waafrika na ipo kwenye nchi zaidi ya 10 Afrika.
Mkurugenzi mtendaji TBC Ayoub Rioba (katikati) na Mkurugenzi wa Kwese Free sports wakionesha hati ya makubaliano baina ya vituo hivyo yalilenga kurusha michuano ya kombe la dunia mwaka 2018.
Mkurugenzi mtendaji wa Kwese Free Sports (TV1) Joseph Swai akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kusaini makubaliano hayo.
Hivyo makala TBC, KWESE FREE SPORTS (TV1) KURUSHA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA (FIFA) BURE KWA KISWAHILI
yaani makala yote TBC, KWESE FREE SPORTS (TV1) KURUSHA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA (FIFA) BURE KWA KISWAHILI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TBC, KWESE FREE SPORTS (TV1) KURUSHA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA (FIFA) BURE KWA KISWAHILI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/tbc-kwese-free-sports-tv1-kurusha.html
0 Response to "TBC, KWESE FREE SPORTS (TV1) KURUSHA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA (FIFA) BURE KWA KISWAHILI"
Post a Comment