title : LULU APANGIWA KUFANYA USAFI WIZARA YA MAMBO YA NDANI
kiungo : LULU APANGIWA KUFANYA USAFI WIZARA YA MAMBO YA NDANI
LULU APANGIWA KUFANYA USAFI WIZARA YA MAMBO YA NDANI
*Atakiwa kuripoti kila siku asubuhi, ikitokea akapata ujauzito atapewa likizo
*Ni marufuku kuzungumza na vyombo vya habari ,akitaka kuigiza filamu ruksa
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MKURUGENZI Msaidizi Idara ya Probesheni na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Nsanze amesema mfungwa Na. 1086/2017 Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu amepangiwa kufanya shughuri za usafi wa mazingira katika maeneo ya Wizara hiyo na kwamba atakuwa akifanya usafi kwa saa nne kila siku na atapumzika siku za mapumziko tu.
Nsenza ameitoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akizunguza na Michuzi Blog ambayo ilitaka kufahamu Lulu baada ya kutolewa jela na kutakiwa kufanya shughuli za kijamii, ni kazi gani amepangiwa kuifanya na itakuwa sehemu gani.
Hivyo akijibu swali hilo amesema kuwa Lulu amepangiwa kufanya shughuli za usafi wa mazingira katika eneo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na alianza kufanya shughuli hizo kuanzia Mei 11 mwaka huu na ataendelea na adhabu hiyo hadi pale atakapomaliza kifungo chake cha nje kwa mujibu wa sheria.
"Lulu amepangiwa kufanya shughuli za usafi eneo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, hivyo ataingia asubuhi kufanya kazi hiyo ambapo kila siku atatumia saa nne kwa ajili hiyo na kisha ataendelea kufanya shughuli zake nyingine. Hivyo yupo hapa na ujio wake umefanya idadi ya wafungwa wanaotumikia vifungo vyao nje ya magereza kufikia 10 ambao wanafanya shughuli mbalimbali eneo hili la Wizara ya Mambo ya Ndani.
"Atakapokuwa hapa hakuna upendeleo , hivyo atafanya kazi kama wafungwa wengine kikubwa ni yeye kufanya kazi hiyo kwa ufasini mkubwa na kuendelea kuonesha tabia njema.Hatutauwa tunamsimamia wakati anafanya usafi na bahati nzuri Sheria ya Huduma za jamii imafafanua vizuri kwa wafungwa ambao wanatumikia vifungo vya nje ya gereza,"amesema Nsenza.
Ameongeza kuwa Lulu atafanya kazi hiyo bila malipo yeyote na kusisitiza ni mfungwa kama walivyo wafungwa wengine na isichukuliwe kuwa yeye tu ndio amepata kifungo cha nje kwani wafungwa wa aina hiyo wapo zaidi ya 12000 hapa nchini.
Alipoulizwa muda ambao Lulu atatakiwa kuripoti kwenye eneo lake la kufanya usafi, Nsenza amejibu kuwa atatakiwa kuingia kati ya saa 12 asubuhi, saa moja asubuhi au saa mbili asubuhi kila siku na atafaya usafi kwa saa nne.Amefafanua kwa Siku za Sikukuu atapumzika na pale anapopatwa na tatizo anaweza kuomba ruhusa na ataruhusiwa kwenda anakotaka.
Pia alipoulizwa kama Lulu atatakiwa kulindwa wakati anatumikia kifungo cha nje, Nsenza amejibu kuwa hatalindwa na mtu yeyote kwani kabla ya kupata kifungo hicho ulishafanyika uchunguzi wa kutosha kuhusu tabia yake na wamejiridhisha hana tatizo na hakuna sababu ya kulindwa."Si kwa Lulu tu bali hata kwa wafungwa wengine wa aina yake nao hawalindwi bali wanatimiza wajibu wao bila kushurutishwa."
Kwa mujibu wa Nsenza ni kwamba Lulu amepata adhabu hiyo kutoka na Sheria ya Huduma za Jamii yenye vifungu 16 na kanuni zake zote 67 atatumikia adhabu yake kwa mujibu wa sheria na kufafanuliwa kuwa sheria hiyo imefafanua kila kitu.
Lulu ambaye ametolewa gerezani Mei 12 mwaka huu(Jumamosi) imefahamika iwapo waandishi wa habari watataka kumhoji cha kwanza yeye mwenyewe atatakiwa kukubali na baada ya hapo ataomba ruhusa kwa mamlaka husika ili afanye mahojiano hayo na iwapo hatafanya hivyo kutakuwa na faini inayoanzia Sh. 500, 000.
"Sheria hairuhusu mfungwa kuingiliwa au kuhojiwa na vyombo vya habari lakini iwapo ataridhia mwenyewe atakubaliwa lakini baada ya sababu ambayo imetolewa kuturidhisha kuwa ipo haja ya kuhojiwa.Sheria hii maana yake ni moja haiko tayari kumzonga zonga mfungwa maana inaweza kuonekana ni unyanyapaa dhidi ya mfungwa.Hivyo kuna taratibu za kufuatwa tu,"amesema.
Ameongeza kuwa sheria hiyo imeeleza kuwa mfungwa atatakiwa kutumikia adhabu yake kwa saa nne kwa siku, hivyo kama kuna mambo anataka kufanya ni ruksa huku akisisitiza katika kifungo hicho wapo wafungwa wanaume na wanawake.Hivyo iwapo itatokea mfungwa mwanamke(akiwamo Lulu) amepata ujauzito atapa likizo na baada ya hapo ataendelea kutumikia adhabu yake.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Probesheni na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Nsanze akizungumza na Globu ya jamii kuhusu mfungwa Na. 1086/2017 Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu aliyepangiwa kufanya shughui za usafi wa mazingira katika maeneo ya Wizara hiyo leo jijini Dar as Salaam .(Picha na Emmanuele Massaka wa Globu ya jamii)
Hivyo makala LULU APANGIWA KUFANYA USAFI WIZARA YA MAMBO YA NDANI
yaani makala yote LULU APANGIWA KUFANYA USAFI WIZARA YA MAMBO YA NDANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala LULU APANGIWA KUFANYA USAFI WIZARA YA MAMBO YA NDANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/lulu-apangiwa-kufanya-usafi-wizara-ya.html
0 Response to "LULU APANGIWA KUFANYA USAFI WIZARA YA MAMBO YA NDANI"
Post a Comment