title : RC KGOMA AHIMIZA WAKUU WA WILAYA, WATENDAJI KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUJIKINGA NA EBOLA
kiungo : RC KGOMA AHIMIZA WAKUU WA WILAYA, WATENDAJI KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUJIKINGA NA EBOLA
RC KGOMA AHIMIZA WAKUU WA WILAYA, WATENDAJI KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUJIKINGA NA EBOLA
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emanuel Maganga, amewataka Wakuu wa Wilaya, Watendaji na watushi wa idara ya afya kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa wananchi kujikinga na magonjwa ya mlipuko kama Ebola.
Pia pamoja na kuweka uangalizi katika mipaka kuzuia ugonjwa huo usiingie katika mkoa wa kigoma.
Maagizo hayo aliyatoa jana katika kikao cha kujadili na kupanga mikakati kuhusu njia bora ya kuzuia uingiaji wa ugonjwa wa ebola kutokana na ugonjwa huo kuripotiwa kuwepo katika nchi jirani ya Jamhuri ya kidemocrasia ya Congo na Mkoa huo kuwa na muingiliano wa wafanya biashara kutoka nchi hiyo na wengine kwenda kwaajili ya biashara kusababisha ugonjwa huo kuingia kwa urahisi nchini.Amesema hatamvumilia nkuu wa wilaya yeyote au ntumishi wa afya atakae kuwa sababu ya kuingia kwa ugonjwa huo.
Ameongeza kwani mkoa wa Kigoma umekuwa ukiongoza katika magonjwa mengi ya mlipuko kama kipindu pindu ambapo umekuwa ugonjwa mkubwa mkoani humo." Mkuu yeyote ambae wilayani mwake kutabainika kunaugonjwa wa mlipuko atachukuliwa hatua.
"Wakuu wa wilaya kazi yenu kubwa ni kutoa elimu kwa wananchi na kuwachukulia hatua watendaji wa afya wasiofanya kazi zao kikamilifu ambao wanasababisha magonjwa hayo kuingia nchini ni wakati wa kuanza kukagua vyoo katika vijiji vyenu," amesema.
Aidha Mkuu huyo amesema hayuko tayari kuona wananchi wanashindwa kufanya kazi kutokana na magonjwa ya milipuko kwani kazi kubwa ya viongozi ni kuwahudumia wananchi.Pia na wananchi wasimamiwe kuweza kuzuia magonjwa ya milipuko na hakuna haja ya Mkoa wa Kigoma kuwa masikini lazima juhudi zifanyike kuhakikisha mkoa unakuwa salama.
Baadhi ya Wadau walioshiriki kwenye mkutano huo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia jenerali mstaafu Emanuel Maganga akimkabidhi choo cha Kisasa Mkurugenzi wa Kibondo Juma Mnwele kati ya vyoo 756 kwa niaba ya wakurugenzi wenzake kwa lengo la kuvipeleka mashuleni na katka vituo vya afya kwa lengo la kuepusha na ugonjwa wa kipindu pindu.
Hivyo makala RC KGOMA AHIMIZA WAKUU WA WILAYA, WATENDAJI KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUJIKINGA NA EBOLA
yaani makala yote RC KGOMA AHIMIZA WAKUU WA WILAYA, WATENDAJI KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUJIKINGA NA EBOLA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC KGOMA AHIMIZA WAKUU WA WILAYA, WATENDAJI KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUJIKINGA NA EBOLA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/rc-kgoma-ahimiza-wakuu-wa-wilaya.html
0 Response to "RC KGOMA AHIMIZA WAKUU WA WILAYA, WATENDAJI KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUJIKINGA NA EBOLA"
Post a Comment