title : JINAMIZI LA MUZIKI WA NGOMA AFRICA BAND WAZIDI KUWADATISHA ULAYA
kiungo : JINAMIZI LA MUZIKI WA NGOMA AFRICA BAND WAZIDI KUWADATISHA ULAYA
JINAMIZI LA MUZIKI WA NGOMA AFRICA BAND WAZIDI KUWADATISHA ULAYA
Wasanii wa Kikundi cha "The Ngoma Africa Band" aka FFU-Ughaibuni au Viumbe wa ajabu "Anunnaki Aliens yenye makao yake nchini ujerumani, wakitowa burudani kwa wapenzi wake katika moja la maonesho yake Ulaya.
Unapotaja muziki wa dansi la kiafrika katika tufe la dunia bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya
"The Ngoma Africa Band" aka FFU-Ughaibuni au Viumbe wa ajabu "Anunnaki Aliens yenye makao yake nchini ujerumani uwezi kukosa kuitaja bendi hiyo inayodumu kwa miaka 25 toka kuanzishwa kwake na kiongozi wake mtanzania Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja.
Bendi hiyo na muziki wake wa dansi au "Bongo Dansi" made in Uswahili ndio bendi pekee iliyofanikiwa kuwanasana washabiki katika kila pembe barani ulaya kwa kutumia ulimbo wa mdundo wake wa "Muziki wa Dansi"
Ambao kwa nyumbani Tanzania unaonekana kama unachimbiwa kaburi kwa makusudi lakini kimataifa Ras Makunja na kikosi chake cha Ngoma Africa Band kinapeperusha bendera majukwaani na muziko huo wa dansi kugeuka jinamizi kubwa liliwakaa moyoni na vichwani mashabiki hao wa kimataifa. ni hivi juzi kati tu katika msimu wa joto barani ulaya.
Ngoma Africa band imefanikiwa kutingisha majukwaa makubwa ya Mamling (Austria),Tallinn(Estonia), majukwa makubwa ya ujerumani Brinkenreid Festival,Regensburg Festival,GaiExpo Tubingen,na juzi tu Alafia Festival Hamburg yote yalifunikwa na muzimu wa muziki wa Ngoma Africa Band ambayo kila pembe imekuwa tishio la kimataifa pamoja na kuachia nyimbo nyingi katika santuri au CDs zao single CD mpya
"Awamu ya Tano Uwanjani" ambayo pia imeletwa katika vituo vya redio hapa nchini Tanzania ndio wanayaotamba nayo.
Bendi hiyo iliyobatizwa majina mengi ya kiusanii na washabiki wake likiwemo jina la "Watoto wa Mbwa" (hawabebeki katika pakacha) imekuwa ni tahasisi inayomilikiwa na washabiki na kuongozwa na Kamanda Ras
Makunja ambaye aliwahi kukaliliwa akisema kama angejua ukubwa wa alichokianzisha angechomoa mapema lakini wapi achomoki tena kwa shinikizo la washabiki.
Muziki wa dansi toka uswahilini unakubalika kimataifa bila
kigugumizi,FFU-ughaibu Ngoma Africa band ungana nao at
Hivyo makala JINAMIZI LA MUZIKI WA NGOMA AFRICA BAND WAZIDI KUWADATISHA ULAYA
yaani makala yote JINAMIZI LA MUZIKI WA NGOMA AFRICA BAND WAZIDI KUWADATISHA ULAYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JINAMIZI LA MUZIKI WA NGOMA AFRICA BAND WAZIDI KUWADATISHA ULAYA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/jinamizi-la-muziki-wa-ngoma-africa-band.html
0 Response to "JINAMIZI LA MUZIKI WA NGOMA AFRICA BAND WAZIDI KUWADATISHA ULAYA"
Post a Comment