SADC WATOA MAFUNZO KWA MAAFISA WA SERIKALI

SADC WATOA MAFUNZO KWA MAAFISA WA SERIKALI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SADC WATOA MAFUNZO KWA MAAFISA WA SERIKALI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SADC WATOA MAFUNZO KWA MAAFISA WA SERIKALI
kiungo : SADC WATOA MAFUNZO KWA MAAFISA WA SERIKALI

soma pia


SADC WATOA MAFUNZO KWA MAAFISA WA SERIKALI

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Serikali ya Ujerumani chini ya Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) na Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imeandaa Warsha ya Mafunzo ya Mfumo wa Ufuatialiaji na Tathmini wa SADC (SADC Results Based Online Monitoring and Evaluation System) kwa maafisa wa Serikali na taasisi za umma. Warsha hii inafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam kuanzia tarehe 15 hadi 17 Mei, 2018.

Lengo la warsha hii ni kuwezesha wizara na taasisi mbalimbali za Serikali kufahamu utendaji kazi wa mfumo huu wa SADC ambao unalenga kukusanya taarifa za utekelezaji wa itifaki na programu mbalimbali za maendeleo za SADC ambazo zinatekelezwa ndani ya nchi na kikanda kwa ujumla. 

Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini wa SADC uliridhiwa na Kikao cha Baraza la Mawaziri wa SADC kilichofanyika katika Falme ya Eswatini (Swaziland) mwezi Machi, 2017. Pamoja na mambo mengine, mfumo huu utawezesha pia nchi wanachama kufanya tathmini ya kina ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Maendeleo ya Kanda uliofanyiwa maboresho wa mwaka 2015-2020 (Revised Regional Indicative Strategic Plan, 2005 – 2020). Mpango huu ndio mkakati mkuu (blueprint) unaosimamia programu zote za kisiasa, kiuchumi na kijamii zinazotekelezwa SADC. 
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Balozi Innocent E. Shiyo akifungua Warsha ya Mafunzo ya Mfumo wa Ufuatialiaji na Tathmini wa SADC (SADC Results Based Online Monitoring and Evaluation System) kwa niaba ya Katibu Mkuu Prof. Aldof Mkenda, kulia kwake ni Meneja Mradi kutoka GIZ Bw. Robson Chakwama na wa mwisho ni mmoja wa Wakufunzi wa Warsha hiyo kutoka SADC Bi. Lerato Moleko 

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Wizara kwa kushirikiana na Serikali ya Ujerumani chini ya Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) na Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), yametolewa kwa Maafisa wa Serikali na Taasisi za Umma, tarehe 15 - 17 Mei,2018 katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.
Sehemu ya Maafisa kutoka Wizarani wakifuatilia mafunzo hayo.
Mkutano ukiendelea
Picha ya pamoja baada ya mkutano.



Hivyo makala SADC WATOA MAFUNZO KWA MAAFISA WA SERIKALI

yaani makala yote SADC WATOA MAFUNZO KWA MAAFISA WA SERIKALI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SADC WATOA MAFUNZO KWA MAAFISA WA SERIKALI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/sadc-watoa-mafunzo-kwa-maafisa-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "SADC WATOA MAFUNZO KWA MAAFISA WA SERIKALI"

Post a Comment