title : Jaji Mkuu Awataka Viongozi na Watendaji wa Mahakama Kutenda Haki
kiungo : Jaji Mkuu Awataka Viongozi na Watendaji wa Mahakama Kutenda Haki
Jaji Mkuu Awataka Viongozi na Watendaji wa Mahakama Kutenda Haki
Na Beatrice Lyimo- Maelezo, Dodoma
Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma amewataka viongozi mbalimbali wa mahakama ikiwemo Naibu Wasajili, Mahakimu, Watendaji, Wakuu wa Idara na Vitengo kutenda haki kwa watumishi walio chini yao.
Jaji Mkuu ameyasema hayo leo Mkoani Dodoma wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa baraza la wafanyakazi wa mahakama Tanzania.
“Sisi kama wasimamizi wakuu wa haki nchini tunawajibu mkuu wa kutenda haki kwa watumishi kwa vitendo, ni ukweli usiopingika kwamba kimbilio la mtumishi yeyote aliyefikwa na matatizo ni kwa kongozi wake katika sehemu yake ya kazi, hivyo basi kila kiongozi anapaswa kufungua milango kwa watumishi waliopo chini yake” amesema Jaji Mkuu.
Jaji Mkuu ameongeza kuwa, ubora wa viongozi unapimwa kwa namna wanavyosaidia wafanyakazi walio chini yao, hivyo kuwataka viongozi hao kutokufunga milango yao kwa watumishi wanaowaongoza.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akihutubia Baraza la Wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania leo Jijini Dodoma.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma (katikati) akishiriki kuimba wimbo wa mshikamano kabla ya kufungua Baraza la Wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania leo Jijini Dodoma.
Wajumbe wa menejimenti ya Mahakama ya Tanzania wakishiriki kuimba wimbo wa mshikamano wakati wa kikao cha Baraza la wafanyakazi leo Jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wa Kikao cha Baraza la wafanyakazi kutoka Kanda ya Dar es Salaam wakifuatilia kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania leo Jijini Dodoma.
Wajumbe wa Kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi ambaye ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma.
Wajumbe wa Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania wakifuatilia hotuba ya Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma wakati wa Kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania .
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Mahakama ya Tanzania Bibi Rose Tengu akitoa maelezo ya awali kuhusu Baraza la Wafanyakazi wa Mahakama Tanzania leo Jijini Dodoma.
Hivyo makala Jaji Mkuu Awataka Viongozi na Watendaji wa Mahakama Kutenda Haki
yaani makala yote Jaji Mkuu Awataka Viongozi na Watendaji wa Mahakama Kutenda Haki Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Jaji Mkuu Awataka Viongozi na Watendaji wa Mahakama Kutenda Haki mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/jaji-mkuu-awataka-viongozi-na-watendaji.html
0 Response to "Jaji Mkuu Awataka Viongozi na Watendaji wa Mahakama Kutenda Haki"
Post a Comment