Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) chasaini mkataba wa ushirikiano na Asasi ya Habari za Maendeleo Tanzania (TADIO)

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) chasaini mkataba wa ushirikiano na Asasi ya Habari za Maendeleo Tanzania (TADIO) - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) chasaini mkataba wa ushirikiano na Asasi ya Habari za Maendeleo Tanzania (TADIO), tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) chasaini mkataba wa ushirikiano na Asasi ya Habari za Maendeleo Tanzania (TADIO)
kiungo : Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) chasaini mkataba wa ushirikiano na Asasi ya Habari za Maendeleo Tanzania (TADIO)

soma pia


Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) chasaini mkataba wa ushirikiano na Asasi ya Habari za Maendeleo Tanzania (TADIO)

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kimesaini mkataba wa ushirikiano wa miaka mitatu na Asasi ya Habari za Maendeleo Tanzania (TADIO), ambayo pia ni mtandao wa radio zenye maudhui ya kijamii nchini. Mtandao huu una radio 31 wanachama zilizopo Tanzania bara na visiwani.
 Chini ya mkataba huo, OUT itatumia wataalam wake (wahadhiri) kushiriki katika vipindi mbalimbali vyenye manufaa kwa umma wa watanzania hususan wananchi wanaoishi vijijni, ambapo radio jamii zinafanya shughuli zake. Pia TADIO kupitia radio wanachama, itawajibika kurusha vipindi hivyo kwa lengo la kuchochea mabadiliko chanya. 
Mkataba huo unaipa fursa TADIO kuwa na ofisi zake katika majengo ya Makao Makuu ya Chuo Kikuu Huria, Kinondoni Dar es Salaam. Pia unatoa fursa kwa wanafunzi wa OUT wa taaluma ya habari na mawasiliano, kutumia studio zilizopo katika majengo hayo zinazomilikiwa na TADIO kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.
 Pamoja na kutumia studio hiyo, wanafunzi wa OUT watapata pia nafasi ya kushiriki mafunzo kwa vitendo katika radio wananchama zilizopo katika maeneo mbalimbali nchini.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Prof. Elifas Bisanda akitoa rai juu ya mkataba huo amesema “OUT itatumia mtandao wa radio wanachama wa TADIO kuifikia jamii na kutoa suluhisho la changamoto mbalimbali za kiuchumi na maendeleo zilizopo kwa kuzingatia vigezo vya utafiti.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), Ndg. Prosper Kwigize (wa pili kulia) akizungumza kabla ya kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa miaka mitatu na Chuo Kikuu Huria (OUT) wakati wa hafla fupi iliyofanyika Chuoni hapo jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha UNESCO Bi. Nancy Kaizilege, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Profesa Elifas Bisanda pamoja na Katibu wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), Marco Mipawa (kulia).
Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), Ndg. Prosper Kwigize na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Profesa Elifas Bisanda wakibadilishana hati za mkataba wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Chuo Kikuu Huria (OUT) na TADIO wakati wa hafla fupi iliyofanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Katibu wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), Marco Mipawa (kulia).
Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), Ndg. Prosper Kwigize na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Profesa Elifas Bisanda wakionyesha hati za mkataba wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Chuo Kikuu Huria (OUT) na TADIO mara baada ya kusainiwa wakati wa hafla fupi iliyofanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Katibu wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), Marco Mipawa (kulia).
Picha ya pamoja ya viongozi wa TADIO, UNESCO na OUT baada ya hafla fupi ya utiaji saini wa mkataba wa makubaliano ya ushirikiano baina ya OUT na TADIO. Kutoka kushoto walioketi ni Bi. Nancy Kaizilege (UNESCO), Prof Elifas Bisanda (VC OUT), Prosper Kwigize (Mwenyekiti TADIO) na Marco Mipawa (Katibu TADIO)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



Hivyo makala Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) chasaini mkataba wa ushirikiano na Asasi ya Habari za Maendeleo Tanzania (TADIO)

yaani makala yote Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) chasaini mkataba wa ushirikiano na Asasi ya Habari za Maendeleo Tanzania (TADIO) Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) chasaini mkataba wa ushirikiano na Asasi ya Habari za Maendeleo Tanzania (TADIO) mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/chuo-kikuu-huria-cha-tanzania-out.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) chasaini mkataba wa ushirikiano na Asasi ya Habari za Maendeleo Tanzania (TADIO)"

Post a Comment