title : Tigo Pesa Yapata Uthibitisho wa Huduma za Kifedha Kutoka Shirika la Kimataifa la GSMA
kiungo : Tigo Pesa Yapata Uthibitisho wa Huduma za Kifedha Kutoka Shirika la Kimataifa la GSMA
Tigo Pesa Yapata Uthibitisho wa Huduma za Kifedha Kutoka Shirika la Kimataifa la GSMA
Tigo Pesa, huduma ya kifedha kwa simu za mkononi inayoongoza nchini, imepokea uthibitisho wa kimataifa ujulikanao kama ‘GSMA Mobile Money Certification’.
Uthibitisho huu unatambua uwezo mkubwa wa Tigo Pesa katika kutoa huduma salama, kwa uwazi, za kuaminika na thabiti zinazokuza haki za wateja na kuzuia miamala ya kihalifu.
Tigo Pesa ni moja kati ya watoa huduma za kifedha kwa simu za mkononi wa kwanza kabisa duniani kupokea uthibitisho huu kutoka GSMA.
GSMA Mobile Money Certification’ ni mkakati wa kimataifa unaolenga kuleta huduma za kifedha salama, wazi na thabiti zaidi kwa mamilioni ya watumiaji wa huduma za kifedha kwa simu za mkononi duniani kote. Huku kukiwa na zaidi ya akaunti 690 milioni za fedha kwa simu za mkononi duniani, sekta ya simu za mkononi inaboresha maisha duniani na imewezesha mamilioni ya watu wasiokuwa na akaunti za benki kufikiwa na huduma rasmi za kifedha.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha kwa Simu za Mkononi wa Tigo, Hussein Sayed alisema, “Tigo Pesa inajivunia mchango wake mkubwa katika kufanikisha upatikanaji wa huduma rasmi za kifedha nchini kwa kutoa fursa kwa mamilioni ya Watanzania wasio na huduma za kibenki kuwa sehemu ya mfumo rasmi wa kifedha.’
Uthibitisho huu kutoka GSMA ni ishara tosha kuwa Tigo Pesa imepiga hatua kubwa kuhakikisha kuwa fedha za wateja wetu zipo salama, na kuwa haki zao zinalindwa. Kupitia taratibu zetu za kibiashara tunalenga kutoa huduma zenye viwango vya juu zaidi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Tigo Pesa Yapata Uthibitisho wa Huduma za Kifedha Kutoka Shirika la Kimataifa la GSMA
yaani makala yote Tigo Pesa Yapata Uthibitisho wa Huduma za Kifedha Kutoka Shirika la Kimataifa la GSMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Tigo Pesa Yapata Uthibitisho wa Huduma za Kifedha Kutoka Shirika la Kimataifa la GSMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/tigo-pesa-yapata-uthibitisho-wa-huduma.html
0 Response to "Tigo Pesa Yapata Uthibitisho wa Huduma za Kifedha Kutoka Shirika la Kimataifa la GSMA"
Post a Comment