title : Watumishi Muhimbili Wapigwa msasa Kuhusu Maadili, Rushwa
kiungo : Watumishi Muhimbili Wapigwa msasa Kuhusu Maadili, Rushwa
Watumishi Muhimbili Wapigwa msasa Kuhusu Maadili, Rushwa
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeendesha mafunzo ya siku mbili ambayo yamelenga kuwakumbusha watumishi wa hospitali hiyo kuzingatia sheria ya kupambana na rushwa mahali pa kazi sambamba na maadili katika utumishi wa umma.
Watumishi walikumbushwa kutojihusisha na vitendo vya kutoa na kupokea rushwa pamoja na madhara yanayotokana na vitendo hivyo.
Ofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Bw. Steven Agwanda aliwataka watumishi wa hospitali hiyo kuzingatia maadili kwa sababu makosa mengi ya rushwa yanasababishwa na ukiukwaji wa maadili.
“Kuna uhusiano mkubwa kati ya rushwa na maadili, mtumishi au viongozi hawachukui rushwa kwa sababu hawana hela, hapa tatizo ni ukosefu wa maadili, zikiwamo tamaa ambazo zinasababishwa na watumishi au viongozi,” alisema Agwanda.
Mafunzo hayo ya siku mbili yalifunguliwa na Mkuu wa Idara ya Ajira na Mafunzo, Bw. Abdallah Kiwanga na yaliwalenga wakuu wa vitengo na wasimamizi wa wodi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Ofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Bw. Steven Agwanda akitoa mada katika semina ya siku mbili kuhusu rushwa mahali pa kazi kwa watumishi wa umma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Sehemu ya watumishi wa umma wa Muhimbili wakimsikiliza mtoa mada kwenye semina hiyo.
Sehemu ya watumishi wa umma wa Muhimbili wakimsikiliza mtoa mada kwenye semina hiyo.
Hivyo makala Watumishi Muhimbili Wapigwa msasa Kuhusu Maadili, Rushwa
yaani makala yote Watumishi Muhimbili Wapigwa msasa Kuhusu Maadili, Rushwa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Watumishi Muhimbili Wapigwa msasa Kuhusu Maadili, Rushwa mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/watumishi-muhimbili-wapigwa-msasa.html
0 Response to "Watumishi Muhimbili Wapigwa msasa Kuhusu Maadili, Rushwa"
Post a Comment