title : SERIKALI KUENDELEA KUKOMESHA AJIRA HATARISHI ZA WATOTO
kiungo : SERIKALI KUENDELEA KUKOMESHA AJIRA HATARISHI ZA WATOTO
SERIKALI KUENDELEA KUKOMESHA AJIRA HATARISHI ZA WATOTO
Serikali imedhamiria kuendelea kukomesha ajira hatarishi za watoto ili kuhakikisha kuwa watoto wanalindwa na kuwapa nafasi stahiki kulingana na sheria na kanuni zilizopo nchini.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipohudhuria katika kilele cha Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 28 Aprili ambapo Kitaifa ilifanyika Mkoani Iringa.
Waziri alieleza kuwa, katika mapambano haya ya ajira hatarishi kwa watoto ni moja ya utekelezaji wa kampeni zinazolenga kuharakisha utekeleezaji wa vipaumbele vilivyomo kwenye lengo namba (8) la Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ambalo ni kuboresha mazingira ya wafanyakazi na kukomesha ajira mbaya kwa watoto.
“Tuendelee kupiga vita ajira mbaya kwa watoto kwa kuzingatia kampeni zilizopo hasa ile ya kuboresha mazingira ya wafanyakazi ifikapo mwaka 2030 pamoja na kukomesha ajira mbaya za watoto ifikapo mwaka 2025,” alisema Waziri
Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na baadhi ya washiriki wa maonesho wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani Aprili 28, 2018 iliyoadhimishwa Kitaifa Mkoani Iringa.
Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiangalia mfano wa namna bora ya kumuokoa mfanyakazi pindi apatapo ajari sehemu ya kazi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani Aprili 28, 2018 Iringa.
Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Mzee Juma Nyinge aliyetembelea katika mabanda ya maonesho wakati wa Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani Aprili 28, 2018.
Hivyo makala SERIKALI KUENDELEA KUKOMESHA AJIRA HATARISHI ZA WATOTO
yaani makala yote SERIKALI KUENDELEA KUKOMESHA AJIRA HATARISHI ZA WATOTO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI KUENDELEA KUKOMESHA AJIRA HATARISHI ZA WATOTO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/serikali-kuendelea-kukomesha-ajira.html
0 Response to "SERIKALI KUENDELEA KUKOMESHA AJIRA HATARISHI ZA WATOTO"
Post a Comment