title : JAFO APIGA STOP UCHIMBAJI MCHANGA KATIKA MITO DAR, MADARAJA YALIYOZOLEWA NA MAFURIKO ILALA, KUJENGWA NA JESHI
kiungo : JAFO APIGA STOP UCHIMBAJI MCHANGA KATIKA MITO DAR, MADARAJA YALIYOZOLEWA NA MAFURIKO ILALA, KUJENGWA NA JESHI
JAFO APIGA STOP UCHIMBAJI MCHANGA KATIKA MITO DAR, MADARAJA YALIYOZOLEWA NA MAFURIKO ILALA, KUJENGWA NA JESHI
Na. John Luhende
Mwambawahabari
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Suleiman Jafo amepiga marufuku uchimbaji wa mchanga katika mito mkoani Dar es Salaam ili Kuzuia uharibifu wa mazingira na Kuzuia mito kupanuakingozake na kuvamia makazi ya watu.
Waziri Jafo Ameyasema katika ziara yake ya Wilayani Ilala kutembelea maeneo na miundombinu iliyo atharika na mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam, ambapo alipofika kukagua Daraja lililo so mbwa na Mafuriko mto msimbazi eneo la Ulongoni, amewakutawananchi wakiendelea na shughuli za uchimbaji mchanga na kutangaza marufuku hiyo.
"Mhe. DC nakuagiza kuanzia sasa kamata mtu yeyote utakaye mkuta anachimba mchanga maeneo ya mito, hawa ndiyo wanaosababisha uharibifu huu, serikali inatumia fedha nyingi Sana kujenga Madaraja halafu mtu anachimba tu bila kujali" alisema
Amesema, Serikali inafanya jitihada ya kujenga Madaraja yaliyobomoka ili wananchi waweze kuendelea na shughuli zao za kiuchumi ambapo sasa wanashindwa kuvuka.
"Nimezunguza na Waziri wa Ulinzi ili Jeshi la wananchi watusaidie kuweka Madaraja ya muda wakati tunajiandaa kujenga mengine, wananchi poleni naomba mvumilie kwa muda " alisema
Aidha Jafo ametembelea Kituo cha Mabasi ya Mwendo Kasi UDART katika eneo la Jangwani na kuagiza Mabasi yasiyo egeshwe eneo hilo ili kuepuka uharibifu utakaowaza kusababishwa na Mafuriko.
"Nakumbuka nili agiza Mabasi yasilazwe hapa lakini na Shangaa mafuriko ya juzi niliona Mabasi yana elea, ila nashukuru kwamba mmenieleza kuwa hayo ni mabovu na mmeshaondoa vitu muhimu, sawa." alisema
Hatahivyo, amesema Serikali ipo katika mpangaji wa kuchimba mto msimbazi na eneo la Jangwani hadi Bahari ni ili kuweza kuweka Suruhisho la kudumu la Mafuriko katika eneo hilo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema , amemtembeza Waziri katika maeneo ambapo Madaraja yamesombwa na Maji, katika eneo la Ulongoni A, Ulongoni B na Pugumachinjioni, na kumueleza athari za mafuriko Wilayani humo na kumshukuru kwa hatua alizochukua kuhakikisha mawasiliano yanarejea maeneo ambapo yalikatika.
Hivyo makala JAFO APIGA STOP UCHIMBAJI MCHANGA KATIKA MITO DAR, MADARAJA YALIYOZOLEWA NA MAFURIKO ILALA, KUJENGWA NA JESHI
yaani makala yote JAFO APIGA STOP UCHIMBAJI MCHANGA KATIKA MITO DAR, MADARAJA YALIYOZOLEWA NA MAFURIKO ILALA, KUJENGWA NA JESHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JAFO APIGA STOP UCHIMBAJI MCHANGA KATIKA MITO DAR, MADARAJA YALIYOZOLEWA NA MAFURIKO ILALA, KUJENGWA NA JESHI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/jafo-apiga-stop-uchimbaji-mchanga.html
0 Response to "JAFO APIGA STOP UCHIMBAJI MCHANGA KATIKA MITO DAR, MADARAJA YALIYOZOLEWA NA MAFURIKO ILALA, KUJENGWA NA JESHI"
Post a Comment