title : Mama aliyemuua mwanawe kisiwani Pemba nae afariki dunia
kiungo : Mama aliyemuua mwanawe kisiwani Pemba nae afariki dunia
Mama aliyemuua mwanawe kisiwani Pemba nae afariki dunia
Na Mwandishi wetu Pemba
Mwanamke aliekamatwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mtoto wake katika kijiji cha Wingwi Micheweni Pemba nae amefariki dunia huku Polisi na Hospitali wakitupiana mpira kuhusu mazingira ya kifo chake.
Jeshi la Polisi ambao walikuwa wakimshikilia mwanamke huyo wamesema alifariki akiwa Hospiltalini lakini madaktari wamesema walipompokea mwanamke huyo kutoka kwa Polisi akiwa tayari amefariki dunia.
Kamanda wa polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Haji Khamis Haji amesema waliamua kumpelaka hospitali mwanamke huyo baada kusema amebanwa na mafua ili ende kupatiwa matibabu.
Daktari aliyemfanyia uchunguzi marehemu huyo, Dk Khalfan Said Salum amesema wamempokea mwanamke huyo kutoka kwa jeshi la polisi akiwa tayari ameshafariki dunia.
Amesema wakati anaendelea kumpima marehemu hyo walimkuta akiwa ametokwa na povu jingi mdomoni na hiyo kuchukua sampuli kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Hata hiyo mwandishi wa habari hizi akiwa anatoka katika hospitali ya Micheweni amemuona mtuhumiwa wa pili wa tukio hilo akiwa anapelekwa hospitali kwa kupatiwa matibabu akiwa na ulinzi kutoka jeshi la Polisi.
Hivyo makala Mama aliyemuua mwanawe kisiwani Pemba nae afariki dunia
yaani makala yote Mama aliyemuua mwanawe kisiwani Pemba nae afariki dunia Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mama aliyemuua mwanawe kisiwani Pemba nae afariki dunia mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/mama-aliyemuua-mwanawe-kisiwani-pemba.html
0 Response to "Mama aliyemuua mwanawe kisiwani Pemba nae afariki dunia"
Post a Comment