DC WA BUHIGWE AWAPONGEZA VIJANA KIGOMA KWA KUUENZI MUUNGANO

DC WA BUHIGWE AWAPONGEZA VIJANA KIGOMA KWA KUUENZI MUUNGANO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DC WA BUHIGWE AWAPONGEZA VIJANA KIGOMA KWA KUUENZI MUUNGANO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DC WA BUHIGWE AWAPONGEZA VIJANA KIGOMA KWA KUUENZI MUUNGANO
kiungo : DC WA BUHIGWE AWAPONGEZA VIJANA KIGOMA KWA KUUENZI MUUNGANO

soma pia


DC WA BUHIGWE AWAPONGEZA VIJANA KIGOMA KWA KUUENZI MUUNGANO

Na Rhoda Ezekiel Kigoma ,

MKUU wa Wilaya ya Buhigwe Brigedia Jenerali Marko Gaguti amewapongeza Vijana wa Kigoma kwa kitendo walichokifanya cha kuuenzi Muungano wa Tanzania, kwa kuandaa mchezo wa kirafiki baina ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi na Bodaboda bila kujali itikadi za Vyama vyao.

Pongezi hizo alizitoa jana Mara baada ya Mchezo huo uliofanyika katika Viwanja vya Kawawa Manispaa ya Kigoma ujiji, wakati akitoa zawadi kwa washindi, ambapo vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM waliibuka washindi kwa penati tano kwa nne dhidi ya timu ya Vijana wa Bodaboda na kuwapatia kila timu mbuzi mmoja na mchele kilo 20 kwa ajili ya kudumisha na kuuenzi Muungano.

Brigedia Gaguti alisema Vijana hao wameonesha Mfano mzuri wa kuigwa na wameienzi falsafa ya Muungano kwa kitendo walichokifanya na kuwataka Vijana hao kuendelea kudumisha umoja na mshikamano hata katika maendeleo ili kuhakikisha Mkoa wa Kigoma unasonga mbele,kufanya kazi kwa bidii pamoja na Kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Nitoe pongezi kwa Vijana wa kigoma kwa Viongozi wa UVCCM na Boda boda kwa hili mlilolifanya la kudumisha Muungano na kuuenzi na kuudumisha , lakini kubwa zaidi mmetoa funzo kwa mchezo huu mlioufanyam, hili ni funzo hata kwa vijana wengine na Watanzania wote mnatakiwa kuishi kwa ushirikiano sio kwa michezo tu hata katika Mambo mengine ya maendeleo ili kuendeleza umoja, mshikamano na uzalendo kama Watanzania bila kujali itikadi za Vyama vyetu", alisema Mkuu huyo.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Kigoma Silvia Sigura alisema Wao kama Viongozi wa Vijana walibuni mchezo huo katika sikuku ya Muungano,lengo likiwa ni kuwaunganisha Vijana wa Mkoa wa kigoma kuwa wamoja na kuendeleza ushirikiano katika kuuinua Mkoa wa Kigoma.

Alisema Michezo ni Afya,ni jambo linaloweza kuwaunganisha Vijana kwa umoja na kuendelea kushirikiana katika Mambo mbali mbali,na Kuwaomba Vijana kuendelea kuwa na ushirikiano mzuri  ili kudumisha amani na mshikamano wa Taifa la Watanzania bila kuangalia Vyama vyao na kuendeleza umoja na mshikamano katika kazi na mambo mbali mbali ya Kijamii.

Nao baadhi ya Vijana wa boda boda walioshiriki katika Mchezo huo January Exavery alisema wanaushukuru sana uongozi wa UVCCM mkoa wa Kigoma kwa Kuandaa mchezo huo wa kirafiki na kuomba ushirikiano huo waliouanzisha uendelee na kuwaasa vijana wengine waachane na ushabiki wa Vyama vya siasa kwa kufanya mambo yasiyo na msingi na wafanye kazi.

Alisema Rais anafanya kazi kibwa kuhakikisha Wananchi wanapata hiduma bora na maendeleo na kuwaasa Vijana kiwa Wakati huu ni wakati wa kufanya kazi kwa kushirikiana na sio wakati wa kukaa vijiweni na kuzungumzia siasa zisizo na Maendeleo na Wafanye kazi kwa bidii ilikuondokana na Umasikini.
MKUU wa Wilaya ya Buhigwe Brigedia Jenerali Marko Gaguti akizungumza wakati akiwapongeza Vijana wa Kigoma kwa kuandaa mchezo wa kirafiki baina ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi na Bodaboda bila kujali itikadi za Vyama vyao kwa dhana ya kuuenzi Muungano wa Tanzania, .


Hivyo makala DC WA BUHIGWE AWAPONGEZA VIJANA KIGOMA KWA KUUENZI MUUNGANO

yaani makala yote DC WA BUHIGWE AWAPONGEZA VIJANA KIGOMA KWA KUUENZI MUUNGANO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DC WA BUHIGWE AWAPONGEZA VIJANA KIGOMA KWA KUUENZI MUUNGANO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/dc-wa-buhigwe-awapongeza-vijana-kigoma.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DC WA BUHIGWE AWAPONGEZA VIJANA KIGOMA KWA KUUENZI MUUNGANO"

Post a Comment