title : BRIGEDIA JENERALI MWANGELA AKAGUA MIRADI,AWAASA WATUMISHI WILAYANI SONGWE KUCHAPA KAZI
kiungo : BRIGEDIA JENERALI MWANGELA AKAGUA MIRADI,AWAASA WATUMISHI WILAYANI SONGWE KUCHAPA KAZI
BRIGEDIA JENERALI MWANGELA AKAGUA MIRADI,AWAASA WATUMISHI WILAYANI SONGWE KUCHAPA KAZI
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas E Mwangela jana jioni amehitimisha ziara yake ya siku mbili Wilayani Songwe, ambapo amekagua miradi kumi ya maendeleo na kisha kuzungumza na watumishi na watendaji wa taasisi mbalimbali zilizomo wilayani humo.
Brigedia Jenerali Mwangela akiwa ameambatana na baadhi ya maafisa wa Mkoa wa Songwe akiwemo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe wametoa maelekezo yaliyohusu kuboresha utendaji kazi kwa watumishi wa Wilaya ya Songwe.
Amesema “nimegundua kila ambacho alinieleza Mkuu wa Mkoa aliyestaafu kuhusu wilaya ya Songwe ni sahihi, upungufu alio uona nami pia nimeuona, napenda kusema mlikuwa mnamuona ni yeye Mkali ila mimi nasema alikuwa Mvumilivu”.
Brigedia Jenerali Mwangela amesema hatosita kumsema na kumchukulia hatua mtendaji anayeenda kinyume na sheria na taratibu za utumishi wa umma hivyo basi watumishi hao wabadilike na kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano, watembelee na kukagua miradi inayotekelezwa wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas E Mwangela akikagua ujenzi wa Kituo cha Afya Mbuyuni Wilayani Songwe, kituo hicho kilipokea shilingi milioni 400 kutoka serikali kuu na kinatarjiwa kukamilika mwezi ujao.
Wananchi wa Kata ya Mbuyuni Wilayani Songwe wakijitolea shughuli mbalimbali za ujenzi katika Kituo cha Afya Mbuyuni ambapo serikali kuu ilitoa shilingi milioni 400 na kituo hicho kinatarajiwa kukamilika mwezi ujao.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas E Mwangela akikagua mradi wa maji Mbuyuni ambao ulikamilika mwaka 2014 lakina bado wananchi hawapati maji kutokana na maji katika chanzo hicho kuwa na rangi mbaya, Brigedia Jenerali Mwangela amemuagiza mhandisi wa maji wilayani humo kufaya utafiti wa chanzo kingine haraka.
Hivyo makala BRIGEDIA JENERALI MWANGELA AKAGUA MIRADI,AWAASA WATUMISHI WILAYANI SONGWE KUCHAPA KAZI
yaani makala yote BRIGEDIA JENERALI MWANGELA AKAGUA MIRADI,AWAASA WATUMISHI WILAYANI SONGWE KUCHAPA KAZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BRIGEDIA JENERALI MWANGELA AKAGUA MIRADI,AWAASA WATUMISHI WILAYANI SONGWE KUCHAPA KAZI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/brigedia-jenerali-mwangela-akagua.html
0 Response to "BRIGEDIA JENERALI MWANGELA AKAGUA MIRADI,AWAASA WATUMISHI WILAYANI SONGWE KUCHAPA KAZI"
Post a Comment