title : CSI yatoa msaada wa vifaa tiba kwa wakina mama wajawazito hospitali ya Mnazi Mmoja
kiungo : CSI yatoa msaada wa vifaa tiba kwa wakina mama wajawazito hospitali ya Mnazi Mmoja
CSI yatoa msaada wa vifaa tiba kwa wakina mama wajawazito hospitali ya Mnazi Mmoja
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
TAASISI ya Childbirth Survival International (CSI) imetoa wa vifaa vya akina mama wajawazito ambavyo hutumika wakati wa kujifunga katika Hospitali ya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Lengo la msaada huo ni muendelezo wa CSI wa kuendelea na jitihada zao za kufanikisha uzazi salama nchini huku moja ya jukumu lao kubwa ni kuhakikisha vifo kwa mama mjazito na mtoto mchanga vinapungua au kwisha kabisa.
Akizungumza leo baada ya kukabidhi vifaa hivyo Mmoja wa Waanzilishi na Mkurugenzi Mkazi nchini Tanzania Stella Mpanda amesema wamekuwa na utaratibu wa kusaidia na kutoa vifaa vya kujifungulia katika hospitali mbalimbali na sasa wameona ni vema wakatoa msadaa huo Hospitali ya Mnazimmoja.
"Tumeamua kusaidia vifaa hivi kwani nia yetu ni kuona mama mjazito na mtoto mchanga wanakuwa salama.Vifaa ambavyo tumekabidhi leo vitarahisisha mkunga kuwa na uhakika wa vifaa na hatimaye mama mjazito kujifungua salama.
"Ni vifaa ambavyo vimetimia kwani ndani yake kuna kila kitu kikiwemo kifaa cha Peguine Pum ambayo husaidia kumsafisha mtoto mara tu baada ya kuzaliwa kwani huondoa uchafu ambao huenda ameuvuta.
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Childbirth Survival International (CSI), Stella Mpanda(wa kwanza kulia) akikabidhi msaada wa vifaa vya akina mama wajawazito kwa Dk. Fillo Hyera (wa tatu kushoto) ambavyo hutumika wakati wa kujifunga katika Hospitali ya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Childbirth Survival International (CSI), Stella Mpanda(wa kwanza kulia) akimkabidhi Mama Mjamzito. Yusta Prospa moja ya kifaa tiba ambacho hutumika wakati wa kujifungulia katika Hospitali ya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Dk. Fillo Hyera(kulia) akitoa shukrani kwa uongozi wa Taasisi ya Childbirth Survival International (CSI) mara baada ya kukabidhi vifaa tiba vya wakina mama wajawazito.KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala CSI yatoa msaada wa vifaa tiba kwa wakina mama wajawazito hospitali ya Mnazi Mmoja
yaani makala yote CSI yatoa msaada wa vifaa tiba kwa wakina mama wajawazito hospitali ya Mnazi Mmoja Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CSI yatoa msaada wa vifaa tiba kwa wakina mama wajawazito hospitali ya Mnazi Mmoja mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/csi-yatoa-msaada-wa-vifaa-tiba-kwa.html
0 Response to "CSI yatoa msaada wa vifaa tiba kwa wakina mama wajawazito hospitali ya Mnazi Mmoja"
Post a Comment