title : WAWEKEZAJI WAHIMIZWA KUJENGA VIWANDA VYA KUBANGUA KOROSHO NA KUTENGENEZA MAGUNIA -RC PWANI
kiungo : WAWEKEZAJI WAHIMIZWA KUJENGA VIWANDA VYA KUBANGUA KOROSHO NA KUTENGENEZA MAGUNIA -RC PWANI
WAWEKEZAJI WAHIMIZWA KUJENGA VIWANDA VYA KUBANGUA KOROSHO NA KUTENGENEZA MAGUNIA -RC PWANI
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MKUU wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo, amewahimiza wawekezaji wenye uwezo wa kujenga viwanda vya kubangua korosho na kutengeneza magunia ,kujenga viwanda hivyo ili kuwarahisishia wakulima wa zao hilo .
Aidha amewaasa maafisa ugani mkoani hapo, kuacha kujibweteka maofisini kupigwa viyoyozi na badala yake watoke na kwenda kwa wakulima kutoa elimu mbalimbali za kilimo cha kisasa na chenye tija cha zao hilo.
Alkadhalika, Ndikilo amewataka wakulima wa zao la korosho kufufua mashamba ya korosho pamoja na kupanda miche mipya ya mikorosho ili kuinua zao hilo kimkoa.
Akizindua upandaji wa miche mipya ya mikorosho Ruvu JKT ,Vikuruti wilayani Kibaha Vijiji, alieleza msimu uliopita ulikumbwa na changamoto ya upungufu wa magunia hivyo kuna kila sababu ya kujengwa viwanda hivyo ili mkulima aweze kuwa na uhakika wa kupata magunia.
Mkuu huyo wa mkoa alisema, miaka ya 60/70 mkoa wa Pwani ulikuwa ukizalisha kwa wingi lakini kwasasa mashamba mengi yametelekezwa hivyo kusababisha kushuka kwa kilimo hicho .
“Baadhi ya wakulima walishindwa kupalilia,kuweka dawa na mashamba mengi yalitelekezwa, kutokana na hilo nachukua fursa hii kutoa rai kwa maafisa ugani, mtoke maofisini, mkawaelimishe wakulima wetu kuhusiana na kilimo chenye tija,na muwahimize wapande miche mipya”
Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,Mhandisi Evarist Ndikilo ,akipanda mche mpya wa zao la mkorosho ,wakati wa uzinduzi wa upandaji wa miche mipya ya mikorosho Mkoani hapo ,uliofanyika ,Ruvu Jkt,huko Vikuruti Kibaha Vijijini.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ,Alhaj Majid Mwanga ,akipanda mche mpya wa zao la mkorosho ,wakati wa uzinduzi wa upandaji wa miche mipya ya mikorosho Mkoani hapo ,uliofanyika ,Ruvu Jkt,huko Vikuruti Kibaha Vijijini. Picha na Mwamvua Mwinyi .
Hivyo makala WAWEKEZAJI WAHIMIZWA KUJENGA VIWANDA VYA KUBANGUA KOROSHO NA KUTENGENEZA MAGUNIA -RC PWANI
yaani makala yote WAWEKEZAJI WAHIMIZWA KUJENGA VIWANDA VYA KUBANGUA KOROSHO NA KUTENGENEZA MAGUNIA -RC PWANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAWEKEZAJI WAHIMIZWA KUJENGA VIWANDA VYA KUBANGUA KOROSHO NA KUTENGENEZA MAGUNIA -RC PWANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/wawekezaji-wahimizwa-kujenga-viwanda.html
0 Response to "WAWEKEZAJI WAHIMIZWA KUJENGA VIWANDA VYA KUBANGUA KOROSHO NA KUTENGENEZA MAGUNIA -RC PWANI"
Post a Comment