title : MABADILIKO YA BEI ZA NISHATI YA MAFUTA
kiungo : MABADILIKO YA BEI ZA NISHATI YA MAFUTA
MABADILIKO YA BEI ZA NISHATI YA MAFUTA
Bei za mafuta yanayopitia bandari ya Dar es Salaam zimepungua kwa mwezi wa pili mfululizo na kufikia shilingi 2,120 kwa lita moja ya petroli, 2,080 kwa dizeli na 2,046 kwa mafuta ya taa.
Kwa kila lita kumekuwa na punguzo la shilingi 175 kwa petroli, shilingi 144 kwa dizeli na shilingi 156 kwa mafuta ya taa, kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nistahi na Maji (EWURA) iliyotolewa jana mjini Dodoma. Bei hizo zitaanza kutumika kesho tarehe 6 Februari, 2019.
Hii ina maana pia kwamba kwa mwezi Januari na Februari 2019, bei za rejareja za Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimepungua kwa jumla ya Shilingi 316, Shilingi 356 na Shilingi 323, mtawalia.
Taarifa hiyo imeeleza pia kwamba bei za mafuta yaliyopitia bandari ya Tanga zitaendelea kuwa zile za mwezi uliopita kwa sababu hakukuwa na shehena mpya.
Hali kadhalika, bei za mafuta yaliyopitia bandari ya Mtwara zitaendelea kuwa zile zile zilizotangazwa Januari 25 2019, ambapo petroli ilipungua kwa shilingi 271 na dizeli shilingi 221 kwa lita.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano,
EWURA.
Hivyo makala MABADILIKO YA BEI ZA NISHATI YA MAFUTA
yaani makala yote MABADILIKO YA BEI ZA NISHATI YA MAFUTA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MABADILIKO YA BEI ZA NISHATI YA MAFUTA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/mabadiliko-ya-bei-za-nishati-ya-mafuta.html
0 Response to "MABADILIKO YA BEI ZA NISHATI YA MAFUTA"
Post a Comment