Misri yakubaliana na Tanzania kujenga kiwanda kikubwa cha nyama na ngozi

Misri yakubaliana na Tanzania kujenga kiwanda kikubwa cha nyama na ngozi - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Misri yakubaliana na Tanzania kujenga kiwanda kikubwa cha nyama na ngozi, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Misri yakubaliana na Tanzania kujenga kiwanda kikubwa cha nyama na ngozi
kiungo : Misri yakubaliana na Tanzania kujenga kiwanda kikubwa cha nyama na ngozi

soma pia


Misri yakubaliana na Tanzania kujenga kiwanda kikubwa cha nyama na ngozi

Na. Saja Kigumbe

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amesema serikali za Tanzania na Misri zimekubaliana kuanzishwa kwa kiwanda kikubwa cha nyama na mazao ya ngozi hapa nchini.

Waziri Mpina amebainisha hayo jana Februari 5,2019 ofisini kwake jijini Dodoma mara baada ya kupata ugeni kutoka nchini Misri ukiongozwa na Waziri wa Kilimo wa nchi hiyo Prof. Ezzaldin Aboussteit.

“Tunaenda kujenga kiwanda kikubwa cha kusindika nyama, cha kusindika ngozi, cha kusindika mazao ya ngozi, kiwanda ambacho hakipo katika nchi hizi zote za Afrika ya Mashariki na Kati.” Alisema Mhe. Mpina

Waziri Mpina amemuhakikishia waziri huyo wa Misri kuwa rasilimali za mifugo na uvuvi zilizopo nchini zipo salama na kwamba wizara imekuwa ikifanya jitahada kuhakikisha samaki hawavuliwi kwa njia haramu na hakuna biashara haramu ili kuhakikisha rasilimali hizo zinanufaisha viwanda vya ndani na wawekezaji watakaokuja kuwekeza katika sekta hizo.

Aidha Waziri Mpina amemuarifu Waziri wa Kilimo wa Misri Prof. Ezzaldin Aboussteit kuwa hakuna mifugo inayoruhusiwa kuingia nchini kutoka nje ya nchi bila ya kuwa na vibali na kuwa usimamizi wa nchi katika rasilimali za mifugo na uvuvi uko salama.

Katika kikao hicho kilichoongozwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina, kilihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, makatibu wakuu wa wizara hiyo pamoja na manejimenti ya wizara.
Waziri wa Kilimo wa Misri Prof. Ezzaldin Aboussteit (kulia) akifafanua jambo katika kikao hicho huku akisiskilizwa kwa makini na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallaha Ulega na wajumbe wengine hawapo pichani
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina (wa tatu kushoto) akizungumza ofisini kwake baada ya kutembelewa na ujumbe kutoka Misri ukiongozwa na Waziri wa Kilimo wa nchi hiyo Prof. Ezzaldin Aboussteit


Hivyo makala Misri yakubaliana na Tanzania kujenga kiwanda kikubwa cha nyama na ngozi

yaani makala yote Misri yakubaliana na Tanzania kujenga kiwanda kikubwa cha nyama na ngozi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Misri yakubaliana na Tanzania kujenga kiwanda kikubwa cha nyama na ngozi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/misri-yakubaliana-na-tanzania-kujenga.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Misri yakubaliana na Tanzania kujenga kiwanda kikubwa cha nyama na ngozi"

Post a Comment