title : UVCCM MKOA WA DAR ES SALAAM, WAINGIA KAZINI KUFUATILIA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM
kiungo : UVCCM MKOA WA DAR ES SALAAM, WAINGIA KAZINI KUFUATILIA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM
UVCCM MKOA WA DAR ES SALAAM, WAINGIA KAZINI KUFUATILIA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM
Mwambawahabari
MWENYEKITI Umoja wa Vijana Wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Dar es salaam Bw. Mussa Kilakala ameanza ziara kutembelea Wilaya za Mkoa wa Dar es salaam ambapo leo ameanzia Wilaya ya Temeke na amekutana na kuzungumza na vijana na watumishi wa Manispaa hiyo.
Kilakala amesema kuwa lengo la Ziara hiyo ni kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM katika kutekeleza miradi ya maendeleo ya wananchi na pia kuangalia Umoja wa Vijana unavyofanyika fanya kazi zake.
Akizungumzia upande wa ujasiriamali ameipongeza Wilaya ya hiyo kwa kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wananchi waiopungua Elfu Moja na ameendelea kusema kuwa wajasiriamali hao ni lazima wapewe mitaji ili wautumie ujasiriamali wao katika kuzalisha,na Mwenyekiti anasema sehemu ya pekee ambayo wanaweza kuanzia kama Vijana ili kupata mitaji hiyo ni kutoka kwenye Halmashauri ambapo Vijana wanatakiwa wapewe asilimia 5% ya Mapato ya ndani na ni jukumu lao kama Umoja kutembelea Halmashauri na Idara mbalimbali ili wajue utekelezaji wa Ilani juu ya asilimia 5% hiyo na namna ambavyo Vijana wanaweza kunufaika nayo.
Hata hivyo Kilakala amesema Mkoa wa Dar es salaam umezindua mfumo maalum wa kutambua Vijana wote,ujuzi wao pamoja na shughuli wanazofanya ili takwimu sahihi ziweze kuandaliwa na Vijana wote wanufaike sawasawa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Felix Lyaniva amewataka wa pokea vijana na hao na kuwa hakikisheni kuwa Ilan ya CCM katika Wilaya Temeke inatekelezwa ipasavyo na kwa upande wa usalama wameimeimarisha ulinzi na matukio ya uharifu yamepungua, na kwamba Halmashauri hiyo inatekeleza miradi ya maendeleo.
Hivyo makala UVCCM MKOA WA DAR ES SALAAM, WAINGIA KAZINI KUFUATILIA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM
yaani makala yote UVCCM MKOA WA DAR ES SALAAM, WAINGIA KAZINI KUFUATILIA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UVCCM MKOA WA DAR ES SALAAM, WAINGIA KAZINI KUFUATILIA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/uvccm-mkoa-wa-dar-es-salaam-waingia.html
0 Response to "UVCCM MKOA WA DAR ES SALAAM, WAINGIA KAZINI KUFUATILIA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM"
Post a Comment