title : USAJILI WA WATAALAM WA MAFUTA,GESI WAENDELEA KUFANYWA NA TaESA
kiungo : USAJILI WA WATAALAM WA MAFUTA,GESI WAENDELEA KUFANYWA NA TaESA
USAJILI WA WATAALAM WA MAFUTA,GESI WAENDELEA KUFANYWA NA TaESA
*Ni kwa ajili ya kupata kazi kwenye mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta Tanzania-Uganda
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WAKALA wa Huduma za Ajira Tanzania(TaESA) umetangaza kuanza kwa mchakato wa utambuzi wa Watanzania wenye taaluma na ujuzi katika sekta ya mafuta na gesi ambapo mwisho wa usajili ni Machi 30 mwaka huu.
Mchakato wa utambuzi huo ni kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga nchini.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Boniface Chandaruba amesema kuwa ili kuhakikisha Watanzania wengi wananuifaka na fursa za ajira zitokanazo na mradi wa bomba la mafuta TaESA imepewa jukumu la kuhamasisha wote wenye taaluma na ujuzi nchini katika sekta ya mafuta na gesi wajitokeze.
“Hivyo tunaomba Watanzania wenye sifa kuja kujisajili TaESA ili waweze kuingizwa kwenye kanzidata ya Wakala kwa lengo la kuiwezesha Serikali kubaini idadi halisi ya walio na sifa zinazohitajika na walio tayari kuajiriwa kwenye mradi wa ujenzi wa bomba hilo.
“Usajili huu unafanyika bure ,hivyo tunasisitiza hakuna gharama yoyote itakayotozwa kwa Mtanzania yeyote atakayehitaji kusajiliwa.Maelezo ya kina kuhusu aina ya fursa za ajira zinazotegemewa kutolewa yanapatikana katika tovuti ya Wakala ya www.taesa.go.tz,”amesema .
Chandaruba amesema mchakato wa usajili unafanyika kwa kujaza fomu maalum ambazo zinapatikana kupitia tovuti ya Wakala au kwa kufika kwenye ofisi zao za kanda zilizopo Dar es Salaam,Arusha, Dodoma na Mwanza.Pia amesema fumu hizo zinapatikana kwa barua pepe eacop@taesa.go.tz na kwamba mchakato wa usajili unatarajia kumalizika Machi 30 mwaka huu.
Hivyo makala USAJILI WA WATAALAM WA MAFUTA,GESI WAENDELEA KUFANYWA NA TaESA
yaani makala yote USAJILI WA WATAALAM WA MAFUTA,GESI WAENDELEA KUFANYWA NA TaESA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala USAJILI WA WATAALAM WA MAFUTA,GESI WAENDELEA KUFANYWA NA TaESA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/usajili-wa-wataalam-wa-mafutagesi.html
0 Response to "USAJILI WA WATAALAM WA MAFUTA,GESI WAENDELEA KUFANYWA NA TaESA"
Post a Comment