title : AZAM KUANZA MAZOEZI WAKIMSUBIRI MTIBWA SUGAR
kiungo : AZAM KUANZA MAZOEZI WAKIMSUBIRI MTIBWA SUGAR
AZAM KUANZA MAZOEZI WAKIMSUBIRI MTIBWA SUGAR
Na Agness Francis Globu ya jamii.
KLABU Bingwa Afrika Mashariki na kati Azam FC kesho wanatarajia kuanza rasmi mazoezi ili
kujiandaa zaidi na michuano ya kuwania Kombe la Shirikisho (ASFC)
ambapo watavaana na Mtibwa Sugar katika mchezo huo wa mtoano.
Mchezo huo utakuwa ni wa vuta nikuvute ikiwa kila timu ikihitaji kupata matokeo mazuri ili kusonga mbele zaidi. Mchezo huo utarindima katika
dimba la Uwanja Wa Azam Complex Chamazi Machi 31 mwaka huu jijini Dar es Salaam huku Azam akimkaribisha Mtibwa Sugar .
Ofisa Habari Azam FC Jaffary Iddy amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa baada ya kumaliza mchezo wao wa Ligi dhidi ya Mbao FC ambapo walipata ushindi wa mabao 2-1, kikosi kilikuwa kwenye mapumziko na kesho kinaaanza mazoezi rasmi ili kukabiliana na mchezo wao ujao dhidi ya Mtibwa sugar.
Ambapo katika mtanange huo ataeibuka kidedea ndiyo ataingia Nusu Fainali ambapo Jaffary amesema wanatarajia mchezo kuwa mgumu kwa pande zote mbili kuwa na morali ya kupata ushindi wa aina yoyote ili kutinga fainali na kusonga mbele.
"Mchezo utakuwa mgumu kwa pande zote mbili tunafahamu timu ya Mtibwa na ikiwa kila kikosi kinahitaji ushindi ili kuendelea na mashindano ukizingatia katika mchezo huo lazima mmoja atoke na mwengine asonge mpaka kufikia kilele na kupata mshindi ambaye atakuwa ni muakilishi wa Nchi kombe la shirikisho Barani Afrika,"amesema Jaffary.
Ameongezea vijana wapo vizuri isipokuwa katika mchezo huo watawakosa wachezaji wao Danile Amor(Ghana)na Yakubuku Mohamedi ambao ni majeruhi pamoja na Yahya Zayd aliyeitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars.
Hivyo makala AZAM KUANZA MAZOEZI WAKIMSUBIRI MTIBWA SUGAR
yaani makala yote AZAM KUANZA MAZOEZI WAKIMSUBIRI MTIBWA SUGAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AZAM KUANZA MAZOEZI WAKIMSUBIRI MTIBWA SUGAR mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/azam-kuanza-mazoezi-wakimsubiri-mtibwa.html
0 Response to "AZAM KUANZA MAZOEZI WAKIMSUBIRI MTIBWA SUGAR"
Post a Comment