WAKULIMA WA MIWA WAKOPESHWA MILIONI 550.

WAKULIMA WA MIWA WAKOPESHWA MILIONI 550. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAKULIMA WA MIWA WAKOPESHWA MILIONI 550., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAKULIMA WA MIWA WAKOPESHWA MILIONI 550.
kiungo : WAKULIMA WA MIWA WAKOPESHWA MILIONI 550.

soma pia


WAKULIMA WA MIWA WAKOPESHWA MILIONI 550.


Wakulima 17 wa mashamba ya miwa wilayani Kilosa, wamenufaika na urasimishaji mashamba kwa kutumia hatimiliki za kimila kukopa Sh milioni 550 kutoka Benki ya Maendeleo ya Wakulima; imeelezwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Adam Mgoyi amesema hayo mjini hapa alipozungumzia manufaa ya urasimishaji ardhi na mashamba wilayani hapa unaoratibiwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita).
Alisema kupitia Mkurabita na wadau wengine, wilaya ya Kilosa inanufaika na urasimishaji mashamba na ardhi kwa kuwa umekuwa chachu ya maendeleo na kilimo chenye tija kinachoongeza pato la wananchi na halmashauri kwa jumla.
“Kwa kipindi cha miaka miwili wakulima 17 wa miwa huko Luhembe wametumia urasimishaji wa ekari zao 6,000 za miwa kupata fursa ya kukopa na hivyo wameongeza uzalishaji wa mavuno,” alisema na kuongeza:
“Kama mtu alikuwa anavuna tani 15 hadi 20, sasa anavuna tani 35 hadi 40 na haya ni matokeo ya mitaji yao kukua kutokana na fursa ya ukopaji waliyoipata baada ya Mkurabita kuratibu urasimishaji wa mashamba yao na kwa msingi huo, pato lao limekua na hata pato la halmashauri yetu linaongezeka.”amesema.
Mkuu wa wilaya huyo wa Kilosa alitoa mwito kwa taasisi za fedha zikiwamo benki wilayani humo kuendelea kuzitambua hati za hatimiliki za kimila na kuzitumia kama dhamana ya mikopo kwa kuwa ni hati halali za kisheria zinazotolewa na serikali.


Hivyo makala WAKULIMA WA MIWA WAKOPESHWA MILIONI 550.

yaani makala yote WAKULIMA WA MIWA WAKOPESHWA MILIONI 550. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAKULIMA WA MIWA WAKOPESHWA MILIONI 550. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/wakulima-wa-miwa-wakopeshwa-milioni-550.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAKULIMA WA MIWA WAKOPESHWA MILIONI 550."

Post a Comment