title : TUZO ZA SZIFF KUFANYIKA APRIL MOSI, STAA WA BEINTEHAA NDANI
kiungo : TUZO ZA SZIFF KUFANYIKA APRIL MOSI, STAA WA BEINTEHAA NDANI
TUZO ZA SZIFF KUFANYIKA APRIL MOSI, STAA WA BEINTEHAA NDANI
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Tuzo za Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) zinatarajia kufanyika April Mosi mwaka huu, huku msanii maarufu kutoka nchini India wa tamthilia ya Beintehaa Pritika Rao 'Aliyah' akitarajiwa kuwa mgeni mwalikwa kuja kushuhudia utowaji wa tuzo hizo.
Hayo yamesemwa wakati wa utangazaji wa vipengele vinavyoshindanishwa katika upatikanaji wa washindi wa tuzo hizo vikiwa katika makundi 19 ikiwemo tuzo ya chaguo la watazamaji (viewers Choice Awards).
Akizungumza na wanahabari Mkurugenzi mtendaji wa Azam Media Tido Mhando amesema kuwa SZIFF ni tuzo za kwanza kubwa kabisa kufanyika nchini ikiwa ni katika malengo mojawapo ya kuibua na kuendeleza tasnia ya Sanaa ya maigizo na filamu ambapo filamu shiriki kutoka Tanzania, Kenya, Burundi, Rwanda na DRC Kongo zimeingia kwenye kinyang'anyiro hicho.
"Timu nzima ya tuzo za SZIFF waliweza kupita mikoa yote nchini na waliweza kupata filamu nyingi sana mikoani na hata nje ya nchi ikiwemo Kenya,Burundi,Rwanda na DRC na zikiwa zimeingia katika kinyang'anyiro cha ushiriki wa tuzo hizo kubwa nchini ikiwa ni mara ya kwanza,"amesema Mhando.
Mhando amesema kuwa SZIFF imejikita zaidi katika filamu zenye maudhui ya kiswahili ambapo takribani filamu 143 zilifanikiwa kupambanishwa na kuruka kila siku kupitia chaneli ya Sinema Zetu na watazamaji waliweza kupata fursa ya kupiga kura.
Kwa upande wa Msimamizi wa tuzo za SZIFF Zamaradi Nzowa amesema kuwa tuzo hizi ni kubwa na mbali na washindi kupata tuzo pia wataweza kuondoka na kitita cha pesa taslimu na utambulisho maalumu na kipekee kwenye soko la tasnia ya filamu ukanda wa Afrika Mashariki na Kati pamoja na nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara.
"Tuzo za SZIFF zitaweza kuitangaza nchi yetu sehemu mbalimbali sambamba na lugha ya kiswahili na pia washindi watajinyakulia pesa taslimu kwani filamu zaidi ya 500 ziliweza kuchujwa kwa vigezo vilivyokuwa vimeweka na majaji wetu ambao hawakuweza kutangazwa hadharani," amesema Zamaradi.
Katika kuweza kuwapata washiriki na washindi mbalimbali,Azam Tv waliweza kushirikiana na COSOTA, BASATA pamoja na bodi ya filamu nchini katika safari ya mchakato mzima wa kuwania tuzo za SZIFF ulioanza rasmi Januar Mosi mwaka huu na kumalizika Machi 12 ambapo filamu zaidi ya 500 zilipokelewa na kuchujwa kwa kutumia vigezo vya kisheria na ubora wa maudhui.
Baadhi ya tuzo zinazowaniwa ni pamoja na Best film, best director, best actor, best actress, best commedian na Best screen play. Zingine ni best editing, best original music, best cinematography hizo zikiwa katika filamu ndefu,filamu fupi pamoja na makala.
Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Tido Mhando akizungumza na wanahabari wakati kutangaza vipengele vya tuzo za Sinema Zetu Film Festival (SZIFF) inayotarajiwa kufanyika April Mosi Mwaka huu na muigizaji wa tamthilia ya Beintehaa Pritika Rao 'Aliyah' akitarajiwa kuwa mgeni mwalikwa. Kulia ni Mkurugenzi msaidizi wa Azam Media Jacob Joseph.
Jaji Mkuu wa Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) Martin Mhando akitaja vipengele vyinavyowaniwa katika tuzo hizo zitakazofanyika April Mosi. Kulia ni Msimamizi wa Tuzo hizo Zamaradi Nzowa
Baadhi ya Wana habari wakifuatilia mkutano huo
Msimamizi wa tuzo za Sinema Zetu Film Festival (SZIFF) Zamaradi Nzowa akielezea jambo kwa wanahabari wakati wa utajaji wa vipengele 19 vinavyowaniwa kwenye tuzo hizo
Hivyo makala TUZO ZA SZIFF KUFANYIKA APRIL MOSI, STAA WA BEINTEHAA NDANI
yaani makala yote TUZO ZA SZIFF KUFANYIKA APRIL MOSI, STAA WA BEINTEHAA NDANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TUZO ZA SZIFF KUFANYIKA APRIL MOSI, STAA WA BEINTEHAA NDANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/tuzo-za-sziff-kufanyika-april-mosi-staa.html
0 Response to "TUZO ZA SZIFF KUFANYIKA APRIL MOSI, STAA WA BEINTEHAA NDANI"
Post a Comment