MISS TANZANIA AKABIDHIWA BENDERA KUIWAKILISHA NCHI MASHINDANO YA DUNIA

MISS TANZANIA AKABIDHIWA BENDERA KUIWAKILISHA NCHI MASHINDANO YA DUNIA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MISS TANZANIA AKABIDHIWA BENDERA KUIWAKILISHA NCHI MASHINDANO YA DUNIA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MISS TANZANIA AKABIDHIWA BENDERA KUIWAKILISHA NCHI MASHINDANO YA DUNIA
kiungo : MISS TANZANIA AKABIDHIWA BENDERA KUIWAKILISHA NCHI MASHINDANO YA DUNIA

soma pia


MISS TANZANIA AKABIDHIWA BENDERA KUIWAKILISHA NCHI MASHINDANO YA DUNIA


Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amemkabidhi bendera ya taifa Miss Tanzania (2018) Queen Elizabeth Makune  atayewakilisha taifa katika mashindano ya urembo ya dunia "Miss World" yatayofanyika nchini China.

Akizungumza na vyombo vya habari Mwakyembe amesema kuwa mlimbwende huyo analiwakilisha taifa na amemtaka akawe balozi bora hasa katika kuitangaza lugha adhimu ya Kiswahili pamoja na maadili ya kiafrika.

Aidha Mwakyembe amemshukuru na kumpongeza mkurugenzi wa "The Look" na mwandaaji wa mashindano hayo Basila Mwanukuzi kwa kurudisha heshima ya mashindano hayo na ametenda haki katika katika tasnia hiyo ya ulimwende.Vilevile amewashukuru wadhamini wa mashindano hayo na kusema kuwa wao kama Wizara kwa kushirikiana na waandaaji wa mashindano hayo watahakikisha kuwa tasnia hiyo inaendelea kusimama imara, na kwa washindi na washiriki wa mashindano hayo watachukuliwa na shirika la ndege nchini ili wawe mabalozi wa kulitangaza taifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi na muandaaji wa mashindano hayo Basila Mwanukuzi amesema kuwa tarehe 8 mwezi huu mrembo huyo ataondoka nchini  kuelekea  China ambako mashindano hayo yatafanyika na amewataka wananchi kutoa ushirikiano ili Tanzania ing'are katika mashindano hayo.Mlimbwende anayewakilisha nchi katika mashindano hayo ambaye ni miss Tanzania 2018 Queen Elizabeth Makune amesema kuwa anakwenda China kuwakilisha nchi na amejiandaa vya kutosha na amehaidi kuleta ushindi nyumbani.

Queen Elizabeth ameeleza kuwa atakuwa balozi katika kuitangaza lugha ya Kiswahili akiwa huko pamoja na utamaduni na maadili ya Kitanzania.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akikabidhi Bendera ya Taifa kwa Mshindi wa Miss Tanzania 2018,Queen Elizabeth Makune ambaye anataraji kwenda nchini Uchina katika Mashindano ya Urembo ya Dunia kuiwakilisha Tanzania katika Masuala ya Urimbwende
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, akizungumza na Waandishi wa habari kabla ya kukabidhi Bendera kwa Miss Tanzania 2018 , Queen Elizabeth Makune
 Miss Tanzania 2018 , Queen Elizabeth Makune akiongea na Waandishi wa Habari na kutoa Tumaini kwa Watanzania kuwa atatwaa taji la Urembo la Dunia
 Mkurugenzi wa Shindano la New Miss Tanzania , Basila Mwanukuzi akizungumza na Waandishi juu ya Safri ya Miss Tanzania Uchina na Fursa walizopata Warembo walioshiriki shindano hilo Mwaka huu.
Afisa Uhusiano wa Baraza la Sanaa nchini, (BASATA), Agness Kimwanga akizungumza jambo kwa niaba ya katibu Mkuu wa BASATA wakati wa makabidhiano ya Bendera kwa Miss Tanzania 2018


Hivyo makala MISS TANZANIA AKABIDHIWA BENDERA KUIWAKILISHA NCHI MASHINDANO YA DUNIA

yaani makala yote MISS TANZANIA AKABIDHIWA BENDERA KUIWAKILISHA NCHI MASHINDANO YA DUNIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MISS TANZANIA AKABIDHIWA BENDERA KUIWAKILISHA NCHI MASHINDANO YA DUNIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/miss-tanzania-akabidhiwa-bendera.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MISS TANZANIA AKABIDHIWA BENDERA KUIWAKILISHA NCHI MASHINDANO YA DUNIA"

Post a Comment