title : TPSF, WADAU WAKUTANA KUJADILI MAFANIKIO YA KUONDOLEWA VIKWAZO VYA KIBIASHARA
kiungo : TPSF, WADAU WAKUTANA KUJADILI MAFANIKIO YA KUONDOLEWA VIKWAZO VYA KIBIASHARA
TPSF, WADAU WAKUTANA KUJADILI MAFANIKIO YA KUONDOLEWA VIKWAZO VYA KIBIASHARA
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
TAASISI ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF), imesema vikwanzo vilivyokuwa katika biashara kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki vimepungua na hivyo kuongezeka kwa fursa za kibiashara.
Hayo yamasemwa na Mkurugenzi wa Sera TPSF, Gilliard Telly wakati wa Warsha kuongeza fursa za biashara katika mipaka ulioandaliwa TPSF kwa kushirikiana Taasisi ya Biashara na Uwekezaji ya East Afrika Mashariki (East Afrika Trade & Investiment Hub) iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Telly amesema changamoto zilizokuwepo katika soko biashara katika nchi za Afrika Mashariki zimeondoka kutokana na kufanya utafiti pamoja na kuzungumza na Serikali kuhusu vikwanzo vya biashara katika tozo.
Amesema tozo hizo zilikuwa kwenye mazao ya mchele iliyokuwa asilimia 10 katika soko la Kenya hali inayofanya wafanyabiashara kushindwa kufanya biashara hiyo.“Moja ya changamoto ilikuwa ni kuchelewa kwa taarifa kuwafikia wafanyabishara lakini kwa sasa taarifa zinawafikia kwa wakati,”amesema.
Telly amesema kuondolewa kwa tozo katika bidhaa za Kilimo katika soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki nako kunafanya kuinuka kwa kiuchumi.Amesema kwa upande wa bidhaa za vyakula Tanzania ndio inayolisha Jumuiya ya Afrika Mashariki, hivyo biashara inazidi kukua kwa wafanyabiahara na kutanua masoko.
Mkurugenzi wa Sera Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF), Gilliard Telly akizungumza katika warsha ya kuhitimisha mradi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na mafanikio ya mradi huo leo jijini Dar es Salaam.
.Mchumi wa East Africa Trade & Investiment Hub, Alfred Kombudo akizungumza mazingira ya biashara katika jumuiya ya Afrika Mashari leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Mkurugenzi wa masuala ya Uchumi wa USAID , Michelle Corzine akizungumza kuhusiana na biashara katika soko la Afrika Mashariki.
Mkurugenzi wa Huduma za Jamii, Loius Accaro akizungumza kuhusiana na wafanyabiashara kushiriki katika masoko mbalimbali leo jijini Dar es Salaam. Leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyabiashara na watendaji wa TPSF wakisikiliza maada mbalimbali.
Hivyo makala TPSF, WADAU WAKUTANA KUJADILI MAFANIKIO YA KUONDOLEWA VIKWAZO VYA KIBIASHARA
yaani makala yote TPSF, WADAU WAKUTANA KUJADILI MAFANIKIO YA KUONDOLEWA VIKWAZO VYA KIBIASHARA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TPSF, WADAU WAKUTANA KUJADILI MAFANIKIO YA KUONDOLEWA VIKWAZO VYA KIBIASHARA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/tpsf-wadau-wakutana-kujadili-mafanikio.html
0 Response to "TPSF, WADAU WAKUTANA KUJADILI MAFANIKIO YA KUONDOLEWA VIKWAZO VYA KIBIASHARA"
Post a Comment