title : TAMASHA LA PASAKA KUTIKISA KANDA YA ZIWA,KUANZIA UWANJA WA CCM KIRUMBA APRILI MOSI JIJINI LA MWANZA
kiungo : TAMASHA LA PASAKA KUTIKISA KANDA YA ZIWA,KUANZIA UWANJA WA CCM KIRUMBA APRILI MOSI JIJINI LA MWANZA
TAMASHA LA PASAKA KUTIKISA KANDA YA ZIWA,KUANZIA UWANJA WA CCM KIRUMBA APRILI MOSI JIJINI LA MWANZA
Ni siku nne zimebaki kengele ya Tamasha la Pasaka zinahesabika. Ni Aprili Mosi, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.
Mara nyingi Tamasha la Pasaka limekuwa likifanyika jijini Dar es Salaam safari hii Msama Promotion imeamua kulifanya tamasha hilo Kanda ya Ziwa. Hivyo Pasaka hii, wapenda muziki wa injili wa Kanda ya Ziwa na viunga vyake watapata burudani ya nyimbo za kumsifu na kumtukuza Mungu huku wakipata mahubiri kwa njia ya uinjilisti wa nyimbo.
Aprili Mosi ni CCM Kirumba, Aprili Pili Tamasha la Pasaka litachukua nafasi Uwanja wa Halmashauri, mkoani Simiyu ambako nako watasheherekea kwa nyimbo za injili.
Wakati siku zikikaribia kuelekea Tamasha la Pasaka kwa mkazi wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa jumla ni kuendelea kumuomba Mungu ili aendelee kukupa uzima na afya njema.Waandaaji wa tamasha hilo, Kampuni ya Msama Promotion, mwaka huu wameamua kuweka vionjo tofauti ili kuhakikisha tamasha hilo linafanyika na kuacha historia kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa.
Kila mwanamuziki aliye kwenye chati, nyimbo zake za kumsifu na kumtukuza Mungu zikiwa zinatamba na kusikika, atakuwemo kuburudisha mashabiki wake na kubwa zaidi ni kwamba kuna baadhi ya waimbaji wataimba wakipiga vyombo vya muziki Live ili kuleta ladha na burudani zaidi katika tamasha hilo..
Kwa mujibu wa waandaji wa Tamasha la Pasaka, mwimbaji Rose Muhando atazindua albam yake mpya “Usivunjike Moyo” kati ya waimbaji wengi kutoka hapa nchini Tanzania na nje watakaofanya mambo makubwa katika tamasha hilo.
Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka akizungumza katika moja ya mikutano yake na waandishi wa habari kuelezea maandalizi ya Tamasha hilo litakalofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Aprili 1 na Kwenye uwanja wa Halmashauri mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Mwimbaji Jesca Honore akithibitisha kushiriki katika tamasha hilo kushoto ni Chrstopher Mwahangila mwimbaji mwingine ambaye atashiriki katika tamasha hilo mkoani Mwanza na Simiyu na katikati ni Jimmy Charles mmoja wa waratibu wa tamasha hilo.
Mwimbaji Upendo Nkone akithibitisha kushiriki katika tamasha hilo kushoto ni Mwimbaji Joshua Mlelwa ambaye pia atakuwepo katika tamasha hilo katikati ni Ufo Saro mmoja wa waratibu wa Tamasha hilo.
Mwimbaji Martha Baraka akitibitisha kushiriki katika tamasha hilo kutoka kushoto ni Jimmy Charles mmoja wa waratibu wa Tamasha hilo na katikati ni Mzee Rainfred Masako mmoja wa Viongozi wa Dira TV.
Mwimbaji Christopher Mwahangila akifanya vitu vyake katika moja ya video zake alizowahi kurekodi.
Hivyo makala TAMASHA LA PASAKA KUTIKISA KANDA YA ZIWA,KUANZIA UWANJA WA CCM KIRUMBA APRILI MOSI JIJINI LA MWANZA
yaani makala yote TAMASHA LA PASAKA KUTIKISA KANDA YA ZIWA,KUANZIA UWANJA WA CCM KIRUMBA APRILI MOSI JIJINI LA MWANZA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAMASHA LA PASAKA KUTIKISA KANDA YA ZIWA,KUANZIA UWANJA WA CCM KIRUMBA APRILI MOSI JIJINI LA MWANZA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/tamasha-la-pasaka-kutikisa-kanda-ya.html
0 Response to "TAMASHA LA PASAKA KUTIKISA KANDA YA ZIWA,KUANZIA UWANJA WA CCM KIRUMBA APRILI MOSI JIJINI LA MWANZA"
Post a Comment