title : POLISI WAIMARISHA ULINZI KUELEKEA PASAKA, LASEMA HALI YA USALAMA WA NCHINI SHWARI
kiungo : POLISI WAIMARISHA ULINZI KUELEKEA PASAKA, LASEMA HALI YA USALAMA WA NCHINI SHWARI
POLISI WAIMARISHA ULINZI KUELEKEA PASAKA, LASEMA HALI YA USALAMA WA NCHINI SHWARI
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
JESHI la Polisi nchini limesema hali ya usalama nchini ni shwari na matukio makubwa ya uhalifu wa kutumia silaha yamepungua kwa kiasia kikubwa huku likieleza kipindi hiki cha kuelekea Sikukuu ya Pasaka linawahakikishia wananchi kuwa limejipanga kikamilifu
Taarifa iliyotolewa leo jijii Dar es Salaam na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ,IGP Simon Sirro ameshukuru ushirikiano ambao wananchi wanautoa kwa jeshi hilo ambao umesaidia kupunguza matukio ya uhalifu na nchi kiusalama iko shwari.
"Kiujumla hali ya usalama hapa nchini ni shwari na matukio makubwa ya uhalifu wa kutumia silaha yamepungua kwa kiasi kikubwa na jitihada za kukabiliana na makosa ya usalama barabarani zinaendelea ili kupunguza ajali zinazosababisha vifo na majeruhi kwa raia,"amesema.
Kuhusu maandalizi ya jeshi hilo kuelekea Pasaka,Sirro amesea wamejipanga katika mikoa yote na kuwahakikishia wananchi kuwa jeshi hilo limejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha Sikukuu hiyo inasherekewa kwa amani na utulivu.
"Na hakuna vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyofanyika na pale vitakapojitokeza vitadhibitiwa kwa haraka.Ulinzi utaimarishwa kwenye maeneo yote yakiwemo maeneo ya kuabudia, fukwe, sehemu za starehe na maeneo mengine ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu ili kuhakikisha wananchi wote wanasherekea sikukuu hiyo katika hali ya utulivu,"amesema.
Amewaomba wazazi na walezi kuwa waangalifu kwa watoto wao na kutowaacha kutembea peke yao bila ya kuwa na uangalizi wa karibu."Kwa wanaomilii kumbi za starehe wanatakiwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa kumbi hizo ikiwemo kutoruhusu disko toto na kujaza watu kupita kiasi".
Wakati huohuo Polisi linawatahadharisha wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani hasa kwa madereva wa magari na pikipiki kuepuka kujaza watu kupita kiasi, kubeba mishikaki, kwenda mwendo kasi, kutumia vilevi pamoja na kupiga honi hovyo.
Hivyo makala POLISI WAIMARISHA ULINZI KUELEKEA PASAKA, LASEMA HALI YA USALAMA WA NCHINI SHWARI
yaani makala yote POLISI WAIMARISHA ULINZI KUELEKEA PASAKA, LASEMA HALI YA USALAMA WA NCHINI SHWARI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala POLISI WAIMARISHA ULINZI KUELEKEA PASAKA, LASEMA HALI YA USALAMA WA NCHINI SHWARI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/polisi-waimarisha-ulinzi-kuelekea.html
0 Response to "POLISI WAIMARISHA ULINZI KUELEKEA PASAKA, LASEMA HALI YA USALAMA WA NCHINI SHWARI"
Post a Comment