RC MWANRI: KUANZIA SASA KILA ZAO NI LAZIMA LILIME KITAAALAMU

RC MWANRI: KUANZIA SASA KILA ZAO NI LAZIMA LILIME KITAAALAMU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RC MWANRI: KUANZIA SASA KILA ZAO NI LAZIMA LILIME KITAAALAMU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RC MWANRI: KUANZIA SASA KILA ZAO NI LAZIMA LILIME KITAAALAMU
kiungo : RC MWANRI: KUANZIA SASA KILA ZAO NI LAZIMA LILIME KITAAALAMU

soma pia


RC MWANRI: KUANZIA SASA KILA ZAO NI LAZIMA LILIME KITAAALAMU

SERIKALI  ya Mkoani Tabora imesema kuanzia msimu ujao mazao yote ni lazima yalimwe kwa kuzingatia kanuni za kilimo bora kinachosisitiza matumizi ya mbolea na ujazaji wa mazao kitaaalamu ili kuhakikisha kunakuwa na mavuno mengi ambayo yatawawezesha wakulima kuzalisha ziada ambayo itawasaidia kuwaletea maendeleo yao binafsi.

Kauli hiyo ilitolewa jana Wilayani Kaliua na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akiendelea na  kampeni zake za kuelimisha wakulima wa pamba juu ya matumizi sahihi ya dawa za kuua wadudu waharibifu katika pamba.

Alisema ulimaji wa hivi sasa kwa  wakulima walio wengi hauzingatii ujazaji wa miche(plant population) kitaalamu katika mashamba yao na matumizi ya mbolea jambo linalopelekea kuwepo na mavuno machache katika eneo kubwa shamba hatua ambayo inamfanya mkulima kuwa na mavuno machache.

Kufuatia hatua hiyo Mkuu huyo wa Mkoa alisema kilimo kijacho ni lazima wakulima wote waliopo  Mkoani Tabora walime kilimo kinachowasaidia kuzalisha ziada na kupata fedha kwa ajili ya kupanua kilimo chake na kuboresha maisha yao.

"Kuanzia sasa ni marufuku kwa wakulima kwa Mkoa huu kulima zao lolote iwe mchicha, viazi , mahindi na mazao ya biashara bila kufuata mistari na kujaza mazao katika shamba...siwezi kuendelea kuvumilia wakulima wanaendelea kulima kilimo ambacho hakiwasaidia kupiga hatua na kuondokana na umaskini kwa kuzalisha mazao mengi katika eneo dogo" alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
 Katibu Tawala Wilaya ya Kaliua Michael Nyahinga( wa pili kutoka kushoto) akitoa maelezo jana kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri( wa pili kulia) wakati alipotembelea shamba la pamba la Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama ikiwa ni sehemu ya kuwaelimisha wakulima wa zao juu ya matumizi sahihi ya dawa za kuua wadudu. Wengine ni Mratibu wa Pamba wa Wilaya ya Kaliua Samwel Mushi(kushoto) na Mshauri wa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Modest Kaijage(kulia).
 Mshauri wa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Modest Kaijage(kulia)  akitoa maelezo jana kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri( wa pili kulia) wakati alipotembelea shamba la pamba la Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama ikiwa ni sehemu ya kuwaelimisha wakulima wa zao juu ya matumizi sahihi ya dawa za kuua wadudu. Wengine ni Katibu Tawala Wilaya ya Kaliua Michael Nyahinga(kushoto) na Afisa Tarafa ya Kaliua Bethod Mahenge (wa pili kulia)
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(wa pili kushoto) akizungumza jambo jana kwa Katibu Tawala Wilaya ya Kaliua Michael Nyahinga( kushoto) wakati alipotembelea shamba la pamba la Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama ikiwa ni sehemu ya kuwaelimisha wakulima wa zao juu ya matumizi sahihi ya dawa za kuua wadudu. Wengine ni Afisa Tarafa ya Kaliua Bethod Mahenge(wa pili kulia) na Mshauri wa Kilimo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Modest Kaijage(kushoto). Picha na Tiganya Vincent

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



Hivyo makala RC MWANRI: KUANZIA SASA KILA ZAO NI LAZIMA LILIME KITAAALAMU

yaani makala yote RC MWANRI: KUANZIA SASA KILA ZAO NI LAZIMA LILIME KITAAALAMU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RC MWANRI: KUANZIA SASA KILA ZAO NI LAZIMA LILIME KITAAALAMU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/rc-mwanri-kuanzia-sasa-kila-zao-ni.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "RC MWANRI: KUANZIA SASA KILA ZAO NI LAZIMA LILIME KITAAALAMU"

Post a Comment