TADB YATOA ‘SAPOTI’ KAMPENI YA KITAIFA YA UNYWAJI WA MAZIWA

TADB YATOA ‘SAPOTI’ KAMPENI YA KITAIFA YA UNYWAJI WA MAZIWA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TADB YATOA ‘SAPOTI’ KAMPENI YA KITAIFA YA UNYWAJI WA MAZIWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TADB YATOA ‘SAPOTI’ KAMPENI YA KITAIFA YA UNYWAJI WA MAZIWA
kiungo : TADB YATOA ‘SAPOTI’ KAMPENI YA KITAIFA YA UNYWAJI WA MAZIWA

soma pia


TADB YATOA ‘SAPOTI’ KAMPENI YA KITAIFA YA UNYWAJI WA MAZIWA

Katika kuhamasisha Watanzania wengi wanaongeza hamasa ya unywaji maziwa, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeunga mkono juhudi za Serikali na Bodi ya Maziwa (TDB) nchini kwa kutoa vifaa vitakavyotumika katika Kampeni ya Kitaifa ya Unywaji Maziwa inayotarajia kufanyika Kitaifa mkoani Kagera kuanzia Mei 28 – Juni 1 mwaka huu.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo yaliyofanyika katika Ofisi za TADB jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema kuwa Benki ya Kilimo imeunga mkono Kampeni hiyo kwa kutambua umuhimu wa kuchagiza unywaji wa maziwa nchini kama inavyopendekezwa na Shirika la Afya Duniani.

“Kwa kutambua umuhimu wa Kampeni hii, TADB kwa kushirikiana na TDB na wadau wengi tumeazimia kuhamasisha unywaji wa maziwa ili kufikia viwango vya kimataifa ya unywaji wa maziwa ambao unakadiriwa kufikia walau lita 200 kwa mwaka kutoka 47 za sasa,” alisema.

Aliongeza kwa kutambua umuhimu wa ufugaji wa ng’ombe wa maziwa TADB ilijumuisha mnyororo wa thamani wa Ufugaji wa ng’ombe wa nyama na maziwa kuwa ni miongoni mwa minyororo ya mwanzo inayopatiwa mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani wa mifugo nchini.

Akasisitiza kuwa Benki yake imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa Ufugaji wa Ng’ombe wa Nyama na Maziwa ili kuchagiza juhudi mbalimbali za Serikali katika ustawi wa tasnia ya maziwa nchini.

“Benki inatoa mikopo na kusaidia uwekezaji kwa ajili ya ujenzi, ununuzi wa mitambo na ufungaji wa mitambo ya kuhudumia ng’ombe ikiwemo majosho na mabwawa ya kunyweshea na pamoja na usindikaji wa maziwa kwa ajili ya kuongeza thamani maziwa,” alisema Bw. Assenga.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (kushoto) akiwakaribisha maafisa kutoka Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) walipomtembelea Ofisini kwake kujadiliana juu ya Kampeni ya Kitaifa ya Unywaji Maziwa inayotarajia kufanyika Kitaifa mkoani Kagera kuanzia Mei 28 – Juni 1 mwaka huu. Katikati ni Kaimu Msajili wa Bodi, Dkt. Mayasa Simba na Afisa Habari na Mawasiliano wa TDB, Queenter Mawinda (kulia).
Menejimenti ya TADB ikifuatilia majadiliano hayo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (kushoto) na Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa, Dkt. Mayasa Simba (kulia) kuhusu nafasi ya wadau katika Kampeni ya Kitaifa ya Unywaji Maziwa inayotarajia kufanyika Kitaifa mkoani Kagera kuanzia Mei 28 – Juni 1 mwaka huu.



Hivyo makala TADB YATOA ‘SAPOTI’ KAMPENI YA KITAIFA YA UNYWAJI WA MAZIWA

yaani makala yote TADB YATOA ‘SAPOTI’ KAMPENI YA KITAIFA YA UNYWAJI WA MAZIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TADB YATOA ‘SAPOTI’ KAMPENI YA KITAIFA YA UNYWAJI WA MAZIWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/tadb-yatoa-sapoti-kampeni-ya-kitaifa-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TADB YATOA ‘SAPOTI’ KAMPENI YA KITAIFA YA UNYWAJI WA MAZIWA"

Post a Comment