ESRF YAENDESHA MAFUNZO KWA WASIMAMIZI WA REDIO JAMII

ESRF YAENDESHA MAFUNZO KWA WASIMAMIZI WA REDIO JAMII - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ESRF YAENDESHA MAFUNZO KWA WASIMAMIZI WA REDIO JAMII, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ESRF YAENDESHA MAFUNZO KWA WASIMAMIZI WA REDIO JAMII
kiungo : ESRF YAENDESHA MAFUNZO KWA WASIMAMIZI WA REDIO JAMII

soma pia


ESRF YAENDESHA MAFUNZO KWA WASIMAMIZI WA REDIO JAMII

Vyombo vya habari nchini hususani redio za kijamii zimetakiwa kuandika habari ambazo zinaelezea changamoto ambazo zinawakabili wananchi katika maisha yao ya kila siku na jinsi ambavyo wanaweza kuzitatua.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kuhusu wajibu wa redio za kijamii kwa maendeleo vijinini ambayo yamehusisha wasimamizi wa redio za kijamii na wawakilishi wa Halmashauri wa wilaya hizo ambao wanawakilisha halmashauri zao katika shughuli za uendeshaji wa redio hizo za jamii.

Alisema wanahabari na vyombo vya habari ni muhimu nchini kwa maendeleo ya Taifa lakini kama wasipokuwa makini katika utendaji wao wa kazi kunaweza kuwa na madhara makubwa hivyo ni wajibu wao kuhakikisha wanazingatia maadili ya uandishi wa habari.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (wa kwanza kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura (wa pili kulia) kabla ya kufungua mafunzo ya siku mbili kuhusu wajibu wa redio za kijamii kwa maendeleo vijinini ambayo yamehusisha wasimamizi wa redio za kijamii na wawakilishi wa Halmashauri wa wilaya hizo ambao wanawakilisha halmashauri zao katika shughuli za uendeshaji wa redio hizo za jamii.

Alisema sehemu kubwa ya wananchi ambao wanaishi vijijini hawapati taarifa muhimu zinazohusu maendeleo yao zikiwepo taarifa za kilimo, afya, mazingira na haki za kibadamu hivyo ni wajibu wao kuhakikisha wanaandika habari ambazo wananchi wamekuwa hawazipati kwa muda mrefu.

“Ni jukumu lenu sasa kuhakikisha redio hizo zinatimiza malengo yake hususani katika kumuelimisha wanajamii, kuwajengea uwezo wa kutambua na kupambana na mazingira ili kuinua hali zao za kimaisha,” Mhe. alisema Wambura.

Alisema mafunzo hiyo ni muhimu kwao kama wawakilishi wa redio za kijamii sababu itawapa mbinu ambazo wanaweza kuzitumia ili waweze kujisimamia wao wenyewe bila kuwa tegemezi kwa kuomba fedha kutoka sehemu zingine.
Picha juu na chini ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura akisoma hotuba ya kufungua mafunzo ya siku mbili kuhusu wajibu wa redio za kijamii kwa maendeleo vijinini ambayo yamehusisha wasimamizi wa redio za kijamii na wawakilishi wa Halmashauri wa wilaya hizo ambao wanawakilisha halmashauri zao katika shughuli za uendeshaji wa redio hizo za jamii.

“Natambua changamoto zilizopo katika uendeshaji wa redio za kijamii ambazo ni kama upatikanji wa habari endelevu na zinazolingana na mahitaji ya jamii husika, uhaba wa rasilimali fedha za kuendeshea redio husika, na udhaifu katika usimamizi stahiki wa taasisi hizo lakini kwa hakika mafunzo haya ni muhimu kwa vile yanalenga kutatua changamoto hizo,” alisema Wambura.

Aidha Naibu Waziri Wambura amewashukuru Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa kutoa mafunzo hayo ambayo yatasaidia kujenga Taifa lenye waandishi na wasimamizi wa habari wenye weledi na kazi zao pia mafunzo hayo yanakwenda sambamba na dira ya wizara ya kuwa na Taifa lililohabarishwa vizuri ifikapo 2025.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida amesema mafunzo hayo yamekuja baada ya kufanyika utafiti mwaka 2014 kwa ufadhili wa UNDP, utafiti ambao ulifanyika kwenye wilaya tano nchini na kugundua kuwa njia bora ya upashaji habari katika maeneo hayo ni kwa kutumia redio.

Amesema baada ya matokeo hayo ya utafiti walipendekeza kuanzishwa kwa redio jamii katika maeneo ambayo utafiti ulifanyika ili kurahisisha taarifa mbalimbali za kuelimisha wananchi ambazo zitakuwa chachu kubwa ya maendeleo kuwafikia wananchi kwa urahisi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho katika mafunzo ya siku mbili kuhusu wajibu wa redio za kijamii kwa maendeleo vijinini ambayo yamehusisha wasimamizi wa redio za kijamii na wawakilishi wa Halmashauri wa wilaya hizo ambao wanawakilisha halmashauri zao katika shughuli za uendeshaji wa redio hizo za jamii.



Hivyo makala ESRF YAENDESHA MAFUNZO KWA WASIMAMIZI WA REDIO JAMII

yaani makala yote ESRF YAENDESHA MAFUNZO KWA WASIMAMIZI WA REDIO JAMII Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ESRF YAENDESHA MAFUNZO KWA WASIMAMIZI WA REDIO JAMII mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/esrf-yaendesha-mafunzo-kwa-wasimamizi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "ESRF YAENDESHA MAFUNZO KWA WASIMAMIZI WA REDIO JAMII"

Post a Comment