title : MASAU BWIRE AZUNGUMZIA UZINDUZI JEZI ZA RUVU SHOOTING
kiungo : MASAU BWIRE AZUNGUMZIA UZINDUZI JEZI ZA RUVU SHOOTING
MASAU BWIRE AZUNGUMZIA UZINDUZI JEZI ZA RUVU SHOOTING
Na Ripota Wetu, Globu ya Jamii
MSEMAJI wa Ruvu Shooting Masau Bwire amesema hivi karibuni wamezindua jezi zake za mashabiki.
Amesema uzinduzi uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Happyness Seneda.
"Baada ya uzinduzi huo, jezi za mashabiki wa Ruvu Shooting za nyumbani (Bluu) na za ugenini (Orange), kwa idadi jumla ya jezi 1,000 ziliingizwa sokoni, tayari kwa mauzo, kila jezi moja (ya juu) ikiuzwa kwa Sh.20,000.
"Mheshimiwa Seneda baada ya kuzindua jezi hizo, aliipiga mnada jezi moja iliyonunuliwa kwa fedha taslimu za Kitanzania Sh.100,000," amesema.
Masau amesema jezi zote 1,000 zilizokuwepo kwa ajili ya kuuzwa kwa mashabiki, siku iliyofuata baada ya uzinduzi zilinunuliwa zote kwa kugombaniwa.
Amesema idadi kubwa ya mashabiki waliohitaji kununua jezi hizo walikosa baada ya kununuliwa zote,hivyo ikalazimu uongozi kufanya mazungumzo na mdhamini, Kampuni ya HAWAII PRODUCTS SUPPLIES LTD kupitia maziwa ya Cowbell, moja ya bidhaa wanazozisambaza ili kuagiza jezi nyingine.
"Wadhamini walikubali, tayari wameanza mchakato wa kuagiza jezi 4,000 ulaya kwa ajili ya mashabiki wa Ruvu Shooting," amesema.Amefafanua hitaji la jezi hizo limekuwa kubwa kwani watu mbalimbali, vyama na baadhi ya timu za soka, rafiki wa Ruvu Shooting wamekuwa wakipiga simu kuomba kununua jezi hizo, mfano, chama cha soka Rufiji walitaka jezi 50 ambazo fedha za malipo yake zipo tayari.
"Niwaombe radhi mashabiki wetu kwa kukosa jezi, lakini niwatie moyo kwamba, Mei mwaka huu zitakuwa zimefika, zenye ubora wa hali ya juu sana," amesema.Ameongeza "Katika hali na mazingira hayo, kwa nini TUSIWAPAPASE? Mtapapaswa sana, tumejipanga, tuko vizuri, kwa zamu, kila mmoja ATAPAPASWA," amesema Masau.
Hivyo makala MASAU BWIRE AZUNGUMZIA UZINDUZI JEZI ZA RUVU SHOOTING
yaani makala yote MASAU BWIRE AZUNGUMZIA UZINDUZI JEZI ZA RUVU SHOOTING Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MASAU BWIRE AZUNGUMZIA UZINDUZI JEZI ZA RUVU SHOOTING mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/masau-bwire-azungumzia-uzinduzi-jezi-za.html
0 Response to "MASAU BWIRE AZUNGUMZIA UZINDUZI JEZI ZA RUVU SHOOTING"
Post a Comment