title : KUJISAJILI WCF LENGO NI KUMUONDOLEA MZIGO WA GHARAMA MWAJIRI,KULINDA HAKI ZA MFANYAKAZI: MAVUNDE
kiungo : KUJISAJILI WCF LENGO NI KUMUONDOLEA MZIGO WA GHARAMA MWAJIRI,KULINDA HAKI ZA MFANYAKAZI: MAVUNDE
KUJISAJILI WCF LENGO NI KUMUONDOLEA MZIGO WA GHARAMA MWAJIRI,KULINDA HAKI ZA MFANYAKAZI: MAVUNDE
SERIKALI ya awamu ya tano imedhamiria kwa dhati kuhakikisha wafanyakazi wanalindwa na kupata haki zao pindi wanapopatwa na madhara yatokanayo na kazi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde amesema mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro..
Mheshimiwa Mavunde ameyasema hayo jana (Machi 1, 2018), wakati akiendelea na ziara yake ya kushtukiza ili kuwabaini waajiri ambao bado hawajatekeelza takwa la kisheria linalowataka waajiri wote katika sekta rasmi,(umma na binafsi), waliopo Tanzania Bara kujisajili na kuchangia kwenye Mfuko huo.
Kwa mujibu wa Sheria iliyoanzisha Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, Ikiwa Mwajiri hatajisajili kwenye Mfuko, atakuwa ametenda kosa la jinai kwa mujibu wa kifungu cha 71(4) cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi na akipatikana na hatia adhabu yake ni kulipa faini isiyozidi shilingi milioni 50,000,000 (Milioni Hamsini) au kifungo kisichozidi miaka mitano jela au adhabu zote kwa pamoja, alisema Mhe. Mavunde.
Mheshimiwa Mavunde ambaye alifuatana na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo Bw. Anslem Peter na Kaimu Kamishna kutoka Idara ya Kazi, Bi. Rehema Moyo, alibaini Mkoa wa Kilimanjaro wenye jumla ya Waajiri 1,039 ni waajiri 525 tu ndio wamejisajili huku wengine 514 bado hawajajisajili na Mfuko.
Naibu Waziri ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde(katikati), akiongozana na Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anslem Peter, (kulia) na Mhasibu wa Shule ya Scolastica, Bw.Moshi W.Moshi, wakati wa ziara yake ya kushtukiza shuleni hapo ili kubaini waajiri ambao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa wafanyakazi, (WCF) ambapo ilibainika shule hiyo kubwa mjini Moshi haijatekeleza takwa hilo la kisheria
Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter, (kulia), akijadili jambo na Kaimu Afisa Kazi Mkoa wa Kilimanjaro, Bi.Neema Msyalika na Afsia Mwandamizi wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bw. Sebere Fulgance.
Mhe. Mavunde akizungumza na Mkurugenzi wa Machare Investments, (kulia).
Hivyo makala KUJISAJILI WCF LENGO NI KUMUONDOLEA MZIGO WA GHARAMA MWAJIRI,KULINDA HAKI ZA MFANYAKAZI: MAVUNDE
yaani makala yote KUJISAJILI WCF LENGO NI KUMUONDOLEA MZIGO WA GHARAMA MWAJIRI,KULINDA HAKI ZA MFANYAKAZI: MAVUNDE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KUJISAJILI WCF LENGO NI KUMUONDOLEA MZIGO WA GHARAMA MWAJIRI,KULINDA HAKI ZA MFANYAKAZI: MAVUNDE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/kujisajili-wcf-lengo-ni-kumuondolea.html
0 Response to "KUJISAJILI WCF LENGO NI KUMUONDOLEA MZIGO WA GHARAMA MWAJIRI,KULINDA HAKI ZA MFANYAKAZI: MAVUNDE"
Post a Comment