JENGO LA ABIRIA KIWANJA CHA DODOMA KUBORESHWA

JENGO LA ABIRIA KIWANJA CHA DODOMA KUBORESHWA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa JENGO LA ABIRIA KIWANJA CHA DODOMA KUBORESHWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : JENGO LA ABIRIA KIWANJA CHA DODOMA KUBORESHWA
kiungo : JENGO LA ABIRIA KIWANJA CHA DODOMA KUBORESHWA

soma pia


JENGO LA ABIRIA KIWANJA CHA DODOMA KUBORESHWA

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, ametoa miezi miwili kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), kuhakikisha linakamilisha uboreshaji wa jengo la abiria lililopo katika kiwanja cha ndege cha Dodoma ili kuwezesha jengo hilo kuhudumia abiria wengi zaidi kwa wakati mmoja.

Ametoa agizo hilo, mkoani Dodoma katika hafla ya utiaji saini mkataba wa uboreshaji wa jengo baina na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA) na NHC na kusema kuwa kukamilika kwake kutawezesha abiria zaidi ya 100 kuhudumiwa kwa wakati mmoja ambapo kwa sasa jengo linahudumia abiria 35.

“Mkataba tunaoshuhudia ukisainiwa leo unaitaka NHC kukamilisha mradi huu ndani ya miezi mitatu lakini niagize mradi huu ukamilike ndani ya miezi miwili kwa sababu fedha zipo na cheti mlichonacho cha daraja la kwanza kinaonyesha namna mnavyoweza kufanya kazi hii kwa haraka’ alisema Mhandisi Nditiye.

Aidha Naibu Waziri Mhandisi Nditiye ameitaka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), pamoja na maboresho hayo kuhakikisha inafanya maboresho kwa kujenga maduka ya kubadilishia fedha na bidhaa ili abiria watakaotumia kiwanja hicho hiyo waweze kupata huduma mbalimbali wakati wanaposubiria kupanda ndege.

Ameongeza kuwa Mkoa wa Dodoma kwa sasa ndio Makao Makuu ya Serikali hivyo miradi yote inayotekelezwa chini ya Wizara lazima izingatie viwango na thamani ya fedha ili kuendana na hadhi ya mji.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia), akioneshwa na Meneja Mradi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Mhandisi Focus Kadege, jengo la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Dodoma ambalo litafanyiwa uboreshwaji ili kuweza kuchukua abiria 100 kwa mara moja, Mkoani humo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamuhanga (kushoto), akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Richard Mayongela wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba wa kuboresha jengo la abiria katika kiwanja cha Ndege cha Dodoma.
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma Mjini, Mhe. Antony Mavunde, akitoa hotuba katika hafla ya utiaji saini wa uboreshaji wa jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege Dodoma, Mkoani humo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Richard Mayongela (kushoto waliokaa) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Maagi (kulia waliokaa), wakisaini mkataba wa uboreshaji wa jengo la abiria uliopo katika Kiwanja cha Ndege cha Dodoma, huku wakishuhudiwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa tatu kulia), Katibu Mkuu wa Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Joseph Nyamuhanga (wa tatu kushoto) na viongozi wengine wa Serikali.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Richard Mayongela (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) (kulia), Felix Maagi wakikabidhiana mkataba wa makubaliano ya uboreshaji wa jengo la abiria uliopo katika Kiwanja cha Ndege cha Dodoma mara baada ya kusaini, Mkoani humo. 




Hivyo makala JENGO LA ABIRIA KIWANJA CHA DODOMA KUBORESHWA

yaani makala yote JENGO LA ABIRIA KIWANJA CHA DODOMA KUBORESHWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala JENGO LA ABIRIA KIWANJA CHA DODOMA KUBORESHWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/jengo-la-abiria-kiwanja-cha-dodoma.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "JENGO LA ABIRIA KIWANJA CHA DODOMA KUBORESHWA"

Post a Comment