title : WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KATIKA KATA SITA
kiungo : WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KATIKA KATA SITA
WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KATIKA KATA SITA
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewasihi wapiga kura wote waliojiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na wanaoishi kwenye kata Sita za Tanzania Bara, kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya Jumapili Desemba 2 mwaka huu ili kuwachagua viongozi wanaowataka wawaongoze kwa kipindi cha takribani miaka miwili ijayo.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Semistocles Kaijage wakati akisoma risala ya uchaguzi mdogo wa Udiwani unaohusisha kata za Miteja, Kivinje au Sigino , Somanga na Mitole katika Halmashauri ya Kilwa, kata ya Muhinda katika Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe na Kata ya Nkoanekoli katika Halmashauri ya wilaya ya Meru.
“Wapiga Kura wapatao 31,818 wanatarajiwa kupiga Kura kuwachagua Madiwani katika Kata 6 za Tanzania Bara na uchaguzi huo utafanyika katika Vituo 91 vya Kupigia Kura ambako ndipo Wapiga kura walijiandikishia kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2015. Aliwataka kwenda kupiga kura bila hofu, woga, wasiwasi au ushawishi kwani chini ya Kanuni ya 3.1 (b) ya Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015, Serikali imepewa wajibu wa kuhakikisha kuwa kuna hali ya usalama, amani na utulivu katika kipindi chote cha Uchaguzi.
Mbali na wito huo, Jaji Kaijage aliwataka wananchi, vyama vya Siasa na wadau wote wa uchaguzi kushirikiana ili kuhakikisha kuwa viashiria vya kuvunjika kwa amani na utulivu vinaepukwa ili uchaguzi utakaofanyika uwe huru, wazi na wa haki. Jaji Kaijage alivisisitiza vyama vya siasa kufanya mikutano ya kampeni inatakiwa kufikia mwisho leo Jumamosi saa kumi na mbili kamili (12:00) jioni na baada ya muda huo, vyama, wagombea na mashabiki waache kufanya kampeni za aina yoyote, kama vile kutumia alama za vyama zinazoashiria kampeni, vipeperushi, bendera, mavazi na vitu vingine visivyokubalika katika siku ya Uchaguzi.
“Aidha, wananchi waheshimu Sheria za Nchi wakati wote wa upigaji, kuhesabu, kujumlisha kura na kutangaza matokeo. Pale panapokuwa na malalamiko yoyote ya ukiukwaji wa Sheria na Taratibu za Uchaguzi, malalamiko hayo yafikishwe kwenye mamlaka inayohusika kwa utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa Sheria.”, alisema Jaji Kaijage na kuongeza kuwa:
“Vivyo hivyo, Viongozi wa Vyama vya Siasa, Wagombea au wafuasi wao na wananchi kwa ujumla wajiepushe na vitendo vinavyoweza kusababisha fujo au vurugu katika vituo vya Kupigia, Kuhesabia na Kujumlishia Kura.” Jaji Kaijage aliwataka wapiga kura kuondoka kwenye maeneo ya kituo cha kupigia kura mara baada ya kupiga kura na kujiepusha na mikusanyiko au mikutano katika maeneo ya vituo vya kupigia kura kwani vyama vya siasa vimeweka mawakala vituoni ambao watalinda maslahi ya vyama husika na wagombea wao.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KATIKA KATA SITA
yaani makala yote WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KATIKA KATA SITA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KATIKA KATA SITA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/wananchi-watakiwa-kujitokeza-uchaguzi_1.html
0 Response to "WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KATIKA KATA SITA"
Post a Comment