title : UAE Kujenga Nyumba 55 Kwa Wananchi Waliopata Maafa Unguja na Pemba.
kiungo : UAE Kujenga Nyumba 55 Kwa Wananchi Waliopata Maafa Unguja na Pemba.
UAE Kujenga Nyumba 55 Kwa Wananchi Waliopata Maafa Unguja na Pemba.
Na Miza Kona-Maelezo Zanzibar.
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetiliana saini ya makubaliano na Serikali ya Nchi za Falme za Kiarabu (UAE), kuhusiana na ujenzi wa nyumba kwa ajili ya wananchi ambao makaazi yao yaliharibika kutokana na mvua za masika.
Hafla hiyo ya utilianaji wa saini hiyo umefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga Zanzibar. kati ya Mamlaka ya Mwezi Mwekundu ya UAE itakayoshughulikia ujenzi huo na K amisheni ya Maafa ya Zanzibar.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed, amesema msaada wa ujenzi huo ni matu nda ya ziara iliyofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein katika Nchi za Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu mwezi ulipita.
Katika ziara hiyo, Mfalme wa UAE aliahidi kuisaidia Zanzibar katika sekta mbalimbali za maendel eo na huduma za kijamii.
“Tunaishukuru serikali ya UAE kwa msaada huu mkubwa ambao utazidi kuimarisha uhusiano na udugu uliop o baina ya nchi zetu,”alisema Aboud.
Nae Mkurugunzi wa kamisheni ya kuka biliana na Maafa Shaaban Seif Mohammed, amesema msaada huo utasaidia kuondoa usumbufu wanaopata wananchi katika kipindi cha mvua hasa yanapotokea mafuriko.
“ Wananchi wanaoishi maeneo ya Ziwa M aboga, Mwanakwerekwe na mengine yanayotuwama maji ndio watakaohamishiwa kwenye nyumba hizo ili wakae katika makaazi salama,” alisema.
“ Aidha nyumba zilizojengwa katika m aeneo yenye kupita au kukaa maji tutazivunja ili kukomesha maafa na usumbufu,”alieleza Mkurugenzi huyo.
Mkurugenzi huyo amewataka wananch i kuchukua tahadhari za mapema kwa k uondoka maeneo yanayokaa maji ili kuepuka na hasara na matatizo wakati wa kipindi cha mvua.
Nae mwakilishi kutoka ubalozi wa UA E Mohammed Ibrahim Al-Bahr, amesema serikali ya nchi yake itaen delea kuisaidia Zanzibar kwa kuimarisha huduma za kijamii ikiwemo hospitali na uchimbaji wa visima kwa lengo la kuwasaidia wananchi wake pamoja na kutemaendelea.
Ameishukuru Serikali ya Zanzibar kwa kuwapatia ardhi itakayotumika kujenga nyumba za makaazi ya kudumu kwa ajili ya wananchi waliokumbwa na maafa ili waishi kwa furaha na utulivu.
Mradihuoutahusishanyumba 55 ambapo 30 zitajengwaFukuchaniMkoawaKaska ziniUnguja, nanyengine 25 zitajengwaTumbeMkoawaKaskazini Pemba.
MWISHO.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
Hivyo makala UAE Kujenga Nyumba 55 Kwa Wananchi Waliopata Maafa Unguja na Pemba.
yaani makala yote UAE Kujenga Nyumba 55 Kwa Wananchi Waliopata Maafa Unguja na Pemba. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UAE Kujenga Nyumba 55 Kwa Wananchi Waliopata Maafa Unguja na Pemba. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/uae-kujenga-nyumba-55-kwa-wananchi.html
0 Response to "UAE Kujenga Nyumba 55 Kwa Wananchi Waliopata Maafa Unguja na Pemba."
Post a Comment