title : NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE. KANYASU AIGIZA TFS ITATUE KERO YA USAFIRISHAJI VINYAGO KWA WATALII
kiungo : NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE. KANYASU AIGIZA TFS ITATUE KERO YA USAFIRISHAJI VINYAGO KWA WATALII
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE. KANYASU AIGIZA TFS ITATUE KERO YA USAFIRISHAJI VINYAGO KWA WATALII
LUSUNGU HELELA-WMU
Baada ya malalamiko ya Watalii walio wengi kulazimika kuacha vinyago kwenye viwanja vya ndege walivyokuwa wamevinunua kwenye maduka mbalimbali nchini kutokana na kukosekana kwa vibali kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) hatimaye Naibu Waziri na Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ameiagiza TFS iangalie namna bora ya kutatua tatizo hilo kwa vile limekuwa likiwaletea usumbufu watalii.
Amelibainisha hilo wakati alipokuwa akizungumza kwenye mkutano na Watumishi wa makao makuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, jijini Dar es Salaam. Amefafanu kuwa watalii wengi hununua vinyago hivyo kwenye maduka mbalimbali hapa nchini kama zawadi ya kupeleka nchini kwao lakini wanapofika kwenye viwanja vya ndege kwa ajili ya kusafiri navyo hudaiwa vibali vya kusafirishia vinyago hivyo jambo ambalo huwalazimu kuviacha kutokana na usumbufu wanaoupata.
Amesema jambo hilo limekuwa likiwafanya watalii wengi kuondoka nchini wakiwa wamekasirishwa kutokana na utaratibu huo kutokuwa wazi huku wakiamini kuwa wamedhulumiwa mali yao. Amesema malalamiko hayo sio mazuri licha ya kuwa TFS nia yake ni njema ya kuhakikisha kuwa lazima kuwe na vibali ya kusafirishia vinyago hivyo kwa ajili kuthibiti uharibifu wa misitu.
Naibu Waziri na Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) wakati aliwapotembelea kwa ajili ya kuzungumza nao ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipoteuliwa kushika nyadhifa hiyo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Dos Santos Silayo akiwasilisha taarifa kabla Naibu Waziri na Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu kuzungumza watumishi wa makao makuu wa TFS, jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Dos Santos Silayo akifafanua jambo kabla Naibu Waziri na Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu kuzungumza na Menejimenti ya TFS, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) wakimsikiliza Naibu Waziri na Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu wakati ali[pokuwa akizungumza nao makao makuu ya TFS jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA-MNRT)
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE. KANYASU AIGIZA TFS ITATUE KERO YA USAFIRISHAJI VINYAGO KWA WATALII
yaani makala yote NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE. KANYASU AIGIZA TFS ITATUE KERO YA USAFIRISHAJI VINYAGO KWA WATALII Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE. KANYASU AIGIZA TFS ITATUE KERO YA USAFIRISHAJI VINYAGO KWA WATALII mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/naibu-waziri-wa-maliasili-na-utalii-mhe_14.html
0 Response to "NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE. KANYASU AIGIZA TFS ITATUE KERO YA USAFIRISHAJI VINYAGO KWA WATALII"
Post a Comment