title : RC MORO AUNDA TIMU YA VYOMBO VYA DOLA ILI KUHAKIKI MAJINA YA WAKAZI WALIOLIPWA FEDHA ZA FIDIA KUPISHA MRADI WA BWAWA LA KIDUNDA ILI KUBAINI HARUFU YA MALIPO ‘HEWA’
kiungo : RC MORO AUNDA TIMU YA VYOMBO VYA DOLA ILI KUHAKIKI MAJINA YA WAKAZI WALIOLIPWA FEDHA ZA FIDIA KUPISHA MRADI WA BWAWA LA KIDUNDA ILI KUBAINI HARUFU YA MALIPO ‘HEWA’
RC MORO AUNDA TIMU YA VYOMBO VYA DOLA ILI KUHAKIKI MAJINA YA WAKAZI WALIOLIPWA FEDHA ZA FIDIA KUPISHA MRADI WA BWAWA LA KIDUNDA ILI KUBAINI HARUFU YA MALIPO ‘HEWA’
Na John Nditi, Globu ya Jamii Morogoro
MKUU wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe ameunda timu maalumu inayojumuisha vyombo vya ulinzi na usalama itakayoshirikiana na wataalamu wa uthamini wa Serikali na wenyeviti wa vitongoji vya vijiji vya Bwila Chini na Kiburumo , kata ya Selembala , halmashauri ya wilaya ya Morogoro ili kuhakiki upya majina ya waliolipwa fedha za fidia na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) kwa ajili ya kupisha ujenzi wa mradi wa bawawa la Kidunda .
Mkuu wa mkoa amelazimika kuunda timu hiyo baada ya kusikiliza malalamiko ya wananchi wa vijiji hivyo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Bwila Chini na kuhudhiriwa na mamia ya wananchi wa vijiji hivyo.
Dk Kebwe alisema , ameiunda timu hiyo licha ya pande zote kueleza kwa udani namna zoezi la uhakiki na uthamini wa makazi ya watu wa vitongoji vinane vya vijiji hivyo kuelezwa kuwa zoezi hili lilifanyika kwa uwazi ulioshirikisha wenyeviti wao wa vitongoji na malipo kufanyika baada ya taratibu zote za kisheria kufuatwa.
Kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi waliopewa furasa ya kuuliza maswali wakidai kuwa wapo baadhi ya watu wamelipwa fedha za fidia wakati zi wakazi wa vitongoji vya vijiji hivyo wakiwa hawana nyumba wala mashamba .
“ Nimelazimika niunde timu ya baadhi ya wajumbe wa kamati za ulinzi na usalama itakayoshirikiana na wataalam na viongozi wa serikali za vitongoji kuhakiki majina yote kwa ajili ya kujiridhisha ili kubaini endapo madai ya wananchi yanaukweli ama laa na yakiwa na ukweli hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wahusika” alisema Dk Kebwe.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe ( kushoto) akifungua kikao cha kusikiliza kero za wananchi wa vijiji vya Bwila Chini na Kiburumo , kata ya Selembala , halmashauri ya wilaya ya Morogoro wakati wakiwasilisha changamoto mbalimbali zikiwemo za malipo ya fedha za fidia kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) kwa ajili ya kupisha ujenzi wa mradi wa bawawa la Kidunda
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe ( kushoto) akiwasiliza kero za wananchi wa vijiji vya Bwila Chini na Kiburumo , kata ya Selembala , halmashauri ya wilaya ya Morogoro wakati wakiwasiisha changamoto mbalimbali zikiwemo za malipo ya fedha za fidia kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) kwa ajili ya kupisha ujenzi wa mradi wa bawawa la Kidunda
Sehemu ya wananchi wa vijiji vya Bwila Chini na Kiburumo , kata ya Selembala , halmashauri ya wilaya ya Morogoro wakimsikiliza mkuu mkoa huo Dk Kebwe Stephen Kebwe ( hayupo pichani) wakati akitoa majawabu ya changamoto mbalimbali zikiwemo za malipo ya fedha za fidia kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) kwa ajili ya kupisha ujenzi wa mradi wa bawawa la Kidunda
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Morogoro, Kibena Kingo ( aliyesimama meza kuu) akitoa maenezo ya ufafanuzi mbele ya mkuu wa mkoa huo Dk Kebwe Stephen Kebwe ( hauonekani pichani) kabla ya kusikiliza changamoto za wananchi wa vijiji vya Bwila Chini na Kiburumo , kata ya Selembala , iliyopo kwenye halmashauri hiyo.
Mkazi wa kijiji cha Bwila Chini kata ya Selembala halmashauri ya wilaya ya Morogoro akitoa kero yake kwa mkuu mkoa wa Morogoro Dk Kebwe Stephen Kebwe ( hayupo pichani) wakati wa mkutano wake wa kusikilkiza changamoto mbalimbali za wananchi wa vijiji viwili cha Bwila Chini na Kiburumo ambao wamelipwa fedha za fidia kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) ili kupisha ujenzi wa mradi wa bawawa la Kidunda. Picha na John Nditi. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA
Hivyo makala RC MORO AUNDA TIMU YA VYOMBO VYA DOLA ILI KUHAKIKI MAJINA YA WAKAZI WALIOLIPWA FEDHA ZA FIDIA KUPISHA MRADI WA BWAWA LA KIDUNDA ILI KUBAINI HARUFU YA MALIPO ‘HEWA’
yaani makala yote RC MORO AUNDA TIMU YA VYOMBO VYA DOLA ILI KUHAKIKI MAJINA YA WAKAZI WALIOLIPWA FEDHA ZA FIDIA KUPISHA MRADI WA BWAWA LA KIDUNDA ILI KUBAINI HARUFU YA MALIPO ‘HEWA’ Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC MORO AUNDA TIMU YA VYOMBO VYA DOLA ILI KUHAKIKI MAJINA YA WAKAZI WALIOLIPWA FEDHA ZA FIDIA KUPISHA MRADI WA BWAWA LA KIDUNDA ILI KUBAINI HARUFU YA MALIPO ‘HEWA’ mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/rc-moro-aunda-timu-ya-vyombo-vya-dola.html
0 Response to "RC MORO AUNDA TIMU YA VYOMBO VYA DOLA ILI KUHAKIKI MAJINA YA WAKAZI WALIOLIPWA FEDHA ZA FIDIA KUPISHA MRADI WA BWAWA LA KIDUNDA ILI KUBAINI HARUFU YA MALIPO ‘HEWA’"
Post a Comment