title : Kishapu yafikia lengo upigaji chapa ng’ombe
kiungo : Kishapu yafikia lengo upigaji chapa ng’ombe
Kishapu yafikia lengo upigaji chapa ng’ombe
Na Robert Hokororo- Ofisi ya Mkurugenzi
Halmashauri ya wilaya ya Kishapu imeweza kupiga chapa jumla ya ng’ombe 225,131 katika zoezi la utambuzi na usajili wa mifugo linalofanyika katika kata zote zenye wafugaji wilayani humo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Stephen Magoiga amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu na limeweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa pamoja na kuwepo kwa changamoto kadhaa.Alisema zoezi hilo ni agizo kutoka serikalini na kinachofanyika ni kulitekeleza kwa kiwango kinachotakiwa na kuweza kuwafikia wafugaji katika maeneo mbalimbali katika kata za wilaya hiyo.
“Zoezi la upigaji chapa ng’ombe tulilipokea na tumeweza kulitekeleza ingawa zipo changamoto mbalimbali zikiwemo baadhi ya maeneo kutokuwepo kwa wafugaji tumefanikiwa kuifikia mifugo hiyo,” alisema.Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mifugo Uvuvi katika Halmashauri hiyo, Dk. Alphonce Bagambabyaki alisema Wilaya imeweza kufikia lengo hilo kwa zaidi ya asilimia 75 ya lengo ambalo ni ng’ombe laki tatu.
Mkuu wa Idara ya Mifugo Uvuvi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Dk. Alphonce Bagambabyaki akishiriki katika zoezi la upigaji chapa ng’ombe.
Wananchi wakishiriki katika zoezi la upigaji chapa ng’ombe katiia kijiji cha Wishiteleja kata ya Mondo.
Moja wa ng’ombe akiwa tayari amepigwa chapa katika sehemu ya mguu.
Hivyo makala Kishapu yafikia lengo upigaji chapa ng’ombe
yaani makala yote Kishapu yafikia lengo upigaji chapa ng’ombe Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Kishapu yafikia lengo upigaji chapa ng’ombe mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/kishapu-yafikia-lengo-upigaji-chapa.html
0 Response to "Kishapu yafikia lengo upigaji chapa ng’ombe"
Post a Comment