title : MGANGA MKUU HALMASHAURI YA NZEGA ATUHUMIWA KUKIUKA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA
kiungo : MGANGA MKUU HALMASHAURI YA NZEGA ATUHUMIWA KUKIUKA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA
MGANGA MKUU HALMASHAURI YA NZEGA ATUHUMIWA KUKIUKA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA
Na Editha Shija-Tabora
Mganga mkuu (DMO) wa halmashauri ya wilaya ya nzega mkoani Tabora Dk,Edward Sengo anatuhumiwa kutumia Lugha za kuudhi na kutotoa ushirikiano kwa viongozi na watendaji wa kata ,hali inayoelezwa kusababisha kuwa inadhoofisha huduma za Afya wilayani humo
Tuhuma hizo zilitolewa Jana na diwani wa kata ya Nkiniziwa Angelina Simon Kisasembe katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano ya halmashauri hiyo
Aidha diwani huyo alisema,Mganga huyo amekuwa akikwamisha jitahada na utoaji wa huduma bora za Afya katika kata hiyo kutokana na kauli zake zisizokuwa na mantiki nzuri katika jamii.
Aliongeza kwa kusema kuwa DMO ni kiongozi wa mfano mzuri katika kitengo cha huduma za Afya katika wilaya hiyo kwani anapaswa kushirikiana vizuri na madiwani na watendaji wa kata zote
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Said Shemahonge alipotakiwa kulitolea ufafanuzi jambo hilo alisema kuwa hana taarifa yoyote ile ya malalamiko yanayoelekezwa kwa mtumishi huyo ila aliahidi kulifanyia kazi na atatoa taarifa kwa kikao kijacho cha baraza.
Baadhi ya Madiwani wakiwa kwenye kikao hicho cha Balaza la Madiwani.
Hivyo makala MGANGA MKUU HALMASHAURI YA NZEGA ATUHUMIWA KUKIUKA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA
yaani makala yote MGANGA MKUU HALMASHAURI YA NZEGA ATUHUMIWA KUKIUKA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MGANGA MKUU HALMASHAURI YA NZEGA ATUHUMIWA KUKIUKA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/mganga-mkuu-halmashauri-ya-nzega.html
0 Response to "MGANGA MKUU HALMASHAURI YA NZEGA ATUHUMIWA KUKIUKA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA"
Post a Comment