title : KILOMBERO YAWAWEZESHA MAELFU WAZEE WASIOJIWEZA HUDUMA ZA CHF ILIYOBORESHWA
kiungo : KILOMBERO YAWAWEZESHA MAELFU WAZEE WASIOJIWEZA HUDUMA ZA CHF ILIYOBORESHWA
KILOMBERO YAWAWEZESHA MAELFU WAZEE WASIOJIWEZA HUDUMA ZA CHF ILIYOBORESHWA
Na John Nditi, Kilombero.
HALMASHAURI ya wilaya ya Kilombero , mkoani Morogoro wamewakatia kadi za Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF ) iliyoboreshwa wazee wasiojiweza zaidi ya 7,800 waliopo katika kata 26 ili kuwawezesha kupata huduma bora za matibabu katika vituo vya Afya, Zahanati na hospitali na wategemezi wao.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo , Dennis Londo alisema hayo mbele ya Katibu tawala mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari, kabla ya zoezi la ugawaji kadi za CHF Iliyoboreshwa kwa baadhi ya wazee wapatao 2,100 kutoka vijiji 23 vya kata saba za Tarafa ya Mlimba.
Londo alisema kuwa , hadi sasa kiasi cha Sh milioni 13.3 zimetumika kwa ajili ya mpango wa kuwakatia wazee wasiojiweza bima ya afya ya CHF Iliyoboreshwa.Hata hivyo alisema , halmashauri hiyo imejipanga kuhakikisha wazee wanapatiwa bima ya Afya CHF iliyoboreshwa na lengo ni kuwafikia wazee wasiojiweza zaidi ya 15,000 katika kata zote 26.
“ Halmashauri ya wilaya hii imejipanga vyema na inatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM na miongoni mwa mam ohayo ni kundi la wazee wasiojiweza wamenufaka na huduma ya bima ya afya” alisema Londo.
Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari ( wapili kushoto) akimkabidhi kadi ya bima ya afya ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) Iliyoboreshwa mzee Petro Karubandika mkazi wa kata ya Mlimba , halmashauri ya wilaya ya Kilombero wakati wa zoezi la ugawaji kadi hizo kwa wapatao 2,100 kutoka vijiji 23 vya kata saba za Tarafa ya Mlimba na ( kushoto) ni mkuu wa wilaya ya Kilombero, James Ihunyo na ( watatu kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Kilombero, Dennis Londo.
Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari ( wapili kushoto) akimkabidhi kadi ya bima ya afya ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) Iliyoboreshwa Nelasi Nyingi , mkazi wa kata ya Mlimba , halmashauri ya wilaya ya Kilombero wakati wa zoezi la ugawaji kadi hizo kwa wapatao 2,100 kutoka vijiji 23 vya kata saba za Tarafa ya Mlimba ( kushoto ) ni mkuu wa wilaya ya Kilombero, James Ihunyo na ( watatu kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Kilombero, Dennis Londo.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Kilombero , Dennis Londo ( kulia) akitoa maelezo mafupi ya mapango wa kuwakatia bima ya afya wazee wasiojiweza kwa Katibu tawala mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari ( wapili kutoka kushoto) wakati wa zoezi la ugawaji kadi za CHF Iliyoboreshwa kwa wazee wapatao 2,100 wa vijiji 23 vya kata saba za Tarafa ya Mlimba.
Baadhi ya wazee wa kata saba za tarafa ya Malimba , halmashauri ya wilaya ya Kilombero wakimsikiliza mgeni rasmi Katibu tawala mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari ( hayupo pichani) wakati wa zoezi la ugawaji kadi za CHF Iliyoboreshwa kwa wazee wapatao 2,100 wa vijiji 23 vya kata saba za Tarafa ya Mlimba. ( Picha na John Nditi).
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala KILOMBERO YAWAWEZESHA MAELFU WAZEE WASIOJIWEZA HUDUMA ZA CHF ILIYOBORESHWA
yaani makala yote KILOMBERO YAWAWEZESHA MAELFU WAZEE WASIOJIWEZA HUDUMA ZA CHF ILIYOBORESHWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KILOMBERO YAWAWEZESHA MAELFU WAZEE WASIOJIWEZA HUDUMA ZA CHF ILIYOBORESHWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/kilombero-yawawezesha-maelfu-wazee.html
0 Response to "KILOMBERO YAWAWEZESHA MAELFU WAZEE WASIOJIWEZA HUDUMA ZA CHF ILIYOBORESHWA"
Post a Comment