NIDA yawataka wananchi kutoa taarifa sahihi katika zoezi la vitambulisho

NIDA yawataka wananchi kutoa taarifa sahihi katika zoezi la vitambulisho - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NIDA yawataka wananchi kutoa taarifa sahihi katika zoezi la vitambulisho, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NIDA yawataka wananchi kutoa taarifa sahihi katika zoezi la vitambulisho
kiungo : NIDA yawataka wananchi kutoa taarifa sahihi katika zoezi la vitambulisho

soma pia


NIDA yawataka wananchi kutoa taarifa sahihi katika zoezi la vitambulisho

MAMLAKA ya vitambulisho vya taifa NIDA mkoa wa Dodoma,imewataka wananchi,wageni na wakimbizi wanaoomba vitambulisho vya taifa kuhakikisha wanatoa taarifa sahihi za utambulisho wao huku wakijihakikishia kutokuwa na makosa ya kisarufi ili kurahisisha upatikanaji wa vitambulisho hivyo.Vitambulisho hivyo ni nyaraka nyeti kwa ajili ya ulinzi na usalama wa Tanzania.

Agnes Gelard ambaye ni Ofisa Habari wa nida,aliyasema hayo jijini Dodoma kwenye maadhimisho ya wiki Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambalo lilizinduliwa rasmi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Kangi Lugola.Akizungumza na mwandishi wetu huku alisisitiza kuwa,makosa ya kisarufi yamekuwa ni changamoto kubwa wanayokumbana nayo wanapokuwa wakiandikisha usajili wa vitambulisho hivyo.
Alisema,”kwa kweli makosa ya kisarufi hasa yale yanayotofautisha majina ya wasajiliwa,imekuwa ni mojawapo ya changamoto kubwa kiasi cha kusababisha wengi kuchelewa kupata vitambulisho. Wananchi wengi wanakosea hata majina yao yaani mtu anaitwa Mariam lakini anaandika Maryamu hivyo kutofautiana na majina yake yaliyopo kwenye nyaraka nyingine’,alisema Ofisa huyo huku akiongezea kuwa,

“Kuna suala la pingamizi,wananchi wengi wanasista kutoa taarifa za mapingamizi hasa kwa watu wanaohisiwa kuwa siyo raia halali wa Tanzania lakini wanakuwa wanaogopa kutoa taarifa hizo,nawahakikishia kuwa,pingamizi la siri litaheshimiwa na kubaki kuwa ni siri baina ya nida na mtoa taarifa tu”.

Kuhusu upatikanaji wa vitambulisho,Agnes alisema kuwa,vinapatikana pasikuwa na gharama yoyote huku wahusika wakitakiwa kuhakikisha wanatoa taarifa kamili na sahihi kuepuka kuwekewa pingamizi jambo ambalo litasababisha kuchelewa kupata nyaraka hiyo muhimu.

“Wananchi wote wajue kuwa,vitambulisho hivi vinatumika kila sehemu,yani kusajili simu,upatikanaji wa mikopo ya elimu ya juu,wenzetu wa TASAF wanavitumia kuwatambua wananchi wanaotakiwa kuhakikiwa nao huku pale inapotokea majanga pia hutumika kuwatambua wahusika waliofikwa na madhira kama mafuriko,ukame na majanga mengine yasiyokuwa ya kibinadamu”.

Kuhusiana na utoaji wa vitambulisho kwa mkoa wa Dodoama,Agnes alisema kuwa,tayari wamekwisajili wananchi wengi na kwa sasa wapo kwenye hatua ya kuchakata taarifa hizo huku pia wakipokea mapingamizi ambayo yanatolewa kupitia anwani ya barua pepe,kwenye ofisi za vijiji na hata wengine wanaofika ofisi za nida ambao pia alisema wameonesha uzalendo wao maana wasiposhiriki wataruhusu wasitakiwa kupatiwa.


Hivyo makala NIDA yawataka wananchi kutoa taarifa sahihi katika zoezi la vitambulisho

yaani makala yote NIDA yawataka wananchi kutoa taarifa sahihi katika zoezi la vitambulisho Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NIDA yawataka wananchi kutoa taarifa sahihi katika zoezi la vitambulisho mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/nida-yawataka-wananchi-kutoa-taarifa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "NIDA yawataka wananchi kutoa taarifa sahihi katika zoezi la vitambulisho"

Post a Comment