title : BASATA KUZICHUKULIA HATUA BENDI ZISIZOSAJILIWA
kiungo : BASATA KUZICHUKULIA HATUA BENDI ZISIZOSAJILIWA
BASATA KUZICHUKULIA HATUA BENDI ZISIZOSAJILIWA
BARAZA la Sanaa Tanzania (BASATA) kutatua kero ya wasanii wa dansi kwa kuwachukulia hatua wanamuziki wa ndondo bendi zisizosajiliwa hapa nchini.
Bendi hizo zimejitokeza kwa wingi kufanya shoo kwenye kumbi mbali mbali ya starehe kwa kuimba kopi ya nyimbo za wasanii hao na kusababisha muziki huo kushuka. Akizungumza na Michuzi Blog leo katika Ukumbi wa BASATA Jijini Dar es Salaam, Meneja wa Bendi ya Twanga Pepeta Asha Baraka amesema muziki huo wa dansi umekuwa hauna faida kwao.
Amefafanua hasa wanapokwenda kufanya shoo kwenye makumbi wateja wanakuwa wachache wanakimbilia huko kwenye hizo bendi zilizoibuka kufanya matamasha yasio na kiingilio.
Aidha Asha Baraka amesema"Kwa wasanii wetu pia wapo wanaoshusha muziki huo kwa msanii kutoka kwenye bendi iliyosajiriwa na kujiunga na hizo bendi zisizofahamika kufanya shoo kama kawaida."Badala yake huleta sintofahamu kwa mameneja kuambiwa wamegawanya bendi ikiwa jambo hilo si la kweli," amesema Asha Baraka.
Ameongeza matokeo yake kusababisha kupungua kwa kipato na biashara inakuwa ngumu,kwani hakuna faida inayopatikana kutokana na hawa ndondo bendi waliojitokeza kufanya kazi hiyo.
Wakati huohuo vilevile Mkurugenzi wa MPOAFRIKA Mpondoli Mwakabana, amewataka BASATA kuwapigania huko ngazi za juu ili kuongezewa muda katika shughuli zao za biashara za makumbi ya starehe na itapelekea hata hizo bendi ziweze kukodishwa badala ya ya zile ndondo ambazo huwa kama deiwaka.
Hivyo makala BASATA KUZICHUKULIA HATUA BENDI ZISIZOSAJILIWA
yaani makala yote BASATA KUZICHUKULIA HATUA BENDI ZISIZOSAJILIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BASATA KUZICHUKULIA HATUA BENDI ZISIZOSAJILIWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/basata-kuzichukulia-hatua-bendi.html
0 Response to "BASATA KUZICHUKULIA HATUA BENDI ZISIZOSAJILIWA"
Post a Comment