DR SILAA ATEMA CHECHE BAADA KUAPISHWA

DR SILAA ATEMA CHECHE BAADA KUAPISHWA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DR SILAA ATEMA CHECHE BAADA KUAPISHWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DR SILAA ATEMA CHECHE BAADA KUAPISHWA
kiungo : DR SILAA ATEMA CHECHE BAADA KUAPISHWA

soma pia


DR SILAA ATEMA CHECHE BAADA KUAPISHWA


Balozi mpya wa Tanzania nchini Sweden, Dk Willibrod Slaa ameapishwa leo Februari 16, 2018, Ikulu Dar es Salaam na Rais John Magufuli na kuahidi kuwa utendaji wake utajikita kwenye diplomasia ya uchumi.

Mbali na Dk Slaa ambaye ni katibu mkuu wa zamani wa Chadema, Rais Magufuli pia amemuapisha Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Muhidin Mboweto.

Rais Magufuli alimteua Dk Slaa kuwa balozi Novemba 23, 2017 na tangu wakati huo alikuwa akisubiri kupangiwa kituo chake cha kazi.

Dk Slaa ambaye tangu ajiuzulu wadhifa wake Chadema amekuwa akiishi Canada, alitangaza kuachana na siasa kutokana na kutofautiana na chama chake katika kumpokea Edward Lowassa aliyehamia kutoka CCM na baadaye kupitishwa kuwa mgombea urais kupitia muungano wa Ukawa.

Alisema chama chake hakikutekeleza makubaliano waliyoafikiana ya kuwapokea baadhi ya makada wa CCM akiwamo Lowassa.

Hafla hiyo fupi ya Ikulu ilihudhuliwa na Naibu Waziri Mambo ya Nje, Dk Suzan Kolimba na Mwenyekiti wa Tume ya Maadili, Jaji Harold Nsekela.

“Tangu nikiwa mbunge na wewe ukiwa bungeni, tumepigia kelele sana ubalozi wa kiuchumi na wewe baada ya kuanza mwaka wa pili, umeanzisha mchakato wa spidi kali katika kila eneo ili kufikisha mahali safari ya kuikuza Tanzania kiuchumi,” amesema Dk Slaa,

“Katika ulimwengu wa leo, pamoja na kazi zile nne zilizozoeleka, diplomasia ya sasa ni ya kiuchumi. Ninakushukuru kwa kunipeleka mahali ambapo naweza kutoa mchango wangu.”

Dk Slaa aliahidi kufanya kazi kwa uwezo wake, akili na kwa nafasi yake yote huku akimwomba Mungu amsaidie kufanikisha dhana ya Tanzania ya viwanda.

“Natambua kwamba maendeleo ni safari na safari yoyote unakwenda hatua kwa hatua. Huwezi kusema unakwenda Mbeya, ukaruka dakika ile ile au sekunde ile ile ukafika Mbeya. Unapiga hatua moja, ya pili unapanda kituo cha kwanza cha pili na tatu,” amesema,

“Ahsante Mheshimiwa Rais kwa kuniona, kwa kuniamini na kunipa majukumu haya, naamini sitakuangusha.”

Naye Balozi Mboweto licha ya kumshukuru Rais Magufuli aliahidi kufanya kazi kwa uwezo wake wote kwa bidii kwa weledi na kwa kuzingatia maadili ya utendaji wa serikali.

Akisisitiza diplomasia, Dk Kolimba amewahakikishia  mabalozi hao ushirikiano katika kutimiza adhama hiyo.

“Jukumu kubwa tulilopewa ni kutekeleza diplomasia ya uchumi na kwa nchi ambazo umewapeleka mabalozi hawa najua watatumia uzoefu walio nao na tutawapa ushirikiano wa kutosha,” amesema.

“Tunataka kuwahakikishia mabalozi hawa wawili walioteuliwa leo sisi kama wizara, tutawapa ushirikiano wa kutosha kwa sababu wao watakuwa sehemu ya wizara.


Hivyo makala DR SILAA ATEMA CHECHE BAADA KUAPISHWA

yaani makala yote DR SILAA ATEMA CHECHE BAADA KUAPISHWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DR SILAA ATEMA CHECHE BAADA KUAPISHWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/dr-silaa-atema-cheche-baada-kuapishwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DR SILAA ATEMA CHECHE BAADA KUAPISHWA"

Post a Comment