Umeme wa Stiegler’s Gorge waiva

Umeme wa Stiegler’s Gorge waiva - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Umeme wa Stiegler’s Gorge waiva, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Umeme wa Stiegler’s Gorge waiva
kiungo : Umeme wa Stiegler’s Gorge waiva

soma pia


Umeme wa Stiegler’s Gorge waiva

*Mawaziri, makatibu wakuu washuhudia kazi nzito 

NDOTO ya Rais Dk. John Magufuli ya kuifanya Tanzania inakuwa na uchumi wa kati na wa viwanda huenda ikatimia baada ya timu ya mawaziri na makatibu wakuu wa wizara 14 ambazo zinatekeleza mradi wa umeme wa Stiegler’s Gorge kuona kazi ya ujenzi wa umeme huo inavyokwenda kwa kasi.

Mradi huo wa umeme ambao ni mkubwa kwa historia ya Tanzania unatarajiwa kuzaliwa umeme wa megawati 2,115 ambazo zinatarajiwa kuingizwa kwenye gridi ya Taifa.

Akitoa maelezo kwa kamati hiyo ya mawaziri na makatibu wakuu pamoja na watalaamu katika eneo la mradi huo, Meneja mkuu wa Kampuni Tanzu ya Tanesco- ETDCO, Mhandisi Elangwa Mgheni Abubakar, alisema kwa sasa kazi ya ujenzi inayoendelea na usimika waya maalumu zenye madini ya kopa kutoka katika kituo cha Matambwe hadi kwenye eneo la mradi.

Pamoja na hali hiyo alisema kutokana na ukubwa wa mradi huo wa kihistoria nguzo zitakazotumika kwa mara ya kwanza ni za zege zaidi ya 700. “Mradi mzima utakuwa na nguzo za zege 700 zenye urefu wa milimita 17. Na huu ni mradi wa kwanza kutumia nguzo za aina hii.

“Tunaendelea na ujenzi huu huku tukiwa tumezingatia masharti ya kitaalamu ikiwamo kukata miti bila kuathiri mazingira kutoka usawa wa ndege. Kwa sasa kazi inayoendelea mafundi wanalaza kebo ambayo itazunguka na kupita chini ya reli na daraja. Awamu ya pili itakuwa kama ya ujenzi pia tutaweka kebo. “Hii line itabeba 33 KV na ya pili nayo itakuwa na ukubwa kama huo ambayo ndani yake kuna waya wa kopa pamoja na nyaya zake ambazo ni nzito,” alisema Mhandisi Elangwa
Meneja Mkuu wa Kampuni Tanzu ya Tanesco (ETDCO), Mhandisi Elangwa Mgheni Abubakar, akitoa maelezo kwa mawaziri na makatibu wakuu waliotembelea mradi wa ujenzi wa umeme wa Stiegler’s Gorge, ambao unatarajiwa kuzaliwa megawati 2,115 katika eneo la mradi Selou Mto Rufiji.
Mjumbe wa Kamati ya Usimamizi ya Utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa mtambo wa umeme wa Stiegler’s Gorge, Justus Mtorela, alitoa maelezo kwa mawaziri na makatibu wakuu namna bwawa la umeme likavyojengwa kando ya Mto Rufiji
Mafundi wa Kampuni Tanzu ya Tanesco (ETDCO), wakiendelea na kazi ya usambazaji kebo chini ya ardhi kuelekea kwenye eneo la mitambo ya umeme wa Stiegler’s Gorge.
Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, akifafanua jambo kwa mawaziri wenzake wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, akihoji kuhusu mradi huo kwa Mjumbe wa Kamati ya Usimamizi ya Utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa mtambo wa umeme wa Stiegler’s Gorge, Justus Mtorela. Kulia ni Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani.



Hivyo makala Umeme wa Stiegler’s Gorge waiva

yaani makala yote Umeme wa Stiegler’s Gorge waiva Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Umeme wa Stiegler’s Gorge waiva mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/umeme-wa-stieglers-gorge-waiva.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Umeme wa Stiegler’s Gorge waiva"

Post a Comment