title : RAIS WA SIMBA FC ALAZWA MUHIMBILI
kiungo : RAIS WA SIMBA FC ALAZWA MUHIMBILI
RAIS WA SIMBA FC ALAZWA MUHIMBILI
MWENDESHA Mashtaka Mwandamizi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa ,(Takukuru) , Leonard Swai ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva amelazwa Hospital ya Taifa ya Muhimbili akisumbuliwa na Figo.
Aveva ambaye ni mshtakiwa wa kwanza shtakiwa mwingine katika kesi ya uhujumu uchumi anashtakiwa pamoja na Makamu rais wa klabu ya Simba, Godfrey Nyange 'Kaburu' ambaye alikuwepo mahakamani hapo
Wakili Swai amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.
Amedai, walishachukua maelezo ya mshtakiwa wa pili na kwamba wanaangalia jinsi ya kupata maelezo ya mshtakiwa wa kwanza ambaye kwa sasa ni mgonjwa.Baada ya kueleza hayo Hakimu Nongwa ameaihirisha kesi hiyo hadi February 8,2018 kwaajili ya kutajwa.
Aveva na Kaburu wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha Dola za kimarekani 300,000.
Hivyo makala RAIS WA SIMBA FC ALAZWA MUHIMBILI
yaani makala yote RAIS WA SIMBA FC ALAZWA MUHIMBILI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RAIS WA SIMBA FC ALAZWA MUHIMBILI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/rais-wa-simba-fc-alazwa-muhimbili.html
0 Response to "RAIS WA SIMBA FC ALAZWA MUHIMBILI"
Post a Comment