title : MKUU WA SHULE NA AFISA ELIMU KATA WA INGIA MATAWAN KWA KUTOZA MICHANGO WANAFUNZI
kiungo : MKUU WA SHULE NA AFISA ELIMU KATA WA INGIA MATAWAN KWA KUTOZA MICHANGO WANAFUNZI
MKUU WA SHULE NA AFISA ELIMU KATA WA INGIA MATAWAN KWA KUTOZA MICHANGO WANAFUNZI
Mkuu wa shule ya Sekondari Halisi Jacob Mosha, akiwa katika kikao na Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, ambapo amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi baada ya kubainika akichangisha wanafunzi michango(Picha na John Luhende)
Na John Luhende
Mwambawahabari
Mkuu wa shule ya Sekondari Halisi, iliyopo Kata ya Majohe Jacob Mosha, pamoja Afisa elimu kata ya Majohe Nancy Peter, wamesimamishwa kazi kwa kosa la kuchangisha michango wanafunzi wa shule hiyo shilingi 2500 ya kitambulisho, na Nembo ya shule shilingi 4000.
Akizungumza shuleni hapo, Afisa Elimu wa mkoa wa Dar es Salaam, Hamis Lisu, amesema Mwalimu huyo amesimamishwa ili kupisha uchunguzi.
Lissu , akiwa ameambatana na Afisa Elimu Wilaya Elizabeth Ngonyani, na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Palela Msogela, baada ya kuzungumza na walimu na wanafunzi shuleni hapo wamesema wanapata vitisho kutoka kwa Mkuu huyo kuwa atakaye sema atafukuzwa ama kuhamishwa shule.
Amesema, kuchangia mchango wanafunzi ni kinyume cha Sheria waraka namba 3 wa elimu bila malipo wa mwaka 2016.
"Pamoja na kuwepo waraka huu nimekuta nimewasisitiza walimu kutowachangisha wanafunzi kama vile haitoshi juzi tena baada ya Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe kulizunguza na kulitilia mkazo nimetuma Barua kwa Wakurugenzi kuwataka wote walikuwa wamepewa vibali vya kuchangisha waache mara moja kwakuwa mkuu wa mkoa alivifuta vyote". Amesema Afisa Elimu.
Pamoja na hayo amesema ataunda Kamati ikiongozwa na yeye na Mkurugenzi, itaanza kazi ya uchunguzi Juma tatu tarehe 29 January na Mkuu wa shule na Afisa Elimu kata ili kupisha uchunguzi wa Kamati na pia amemwaagiza Mkurugenzi kutafuta mtu wakukaimu nafasi ya Mratibu kata.
Pia amewataka walimu ambao wanatishiwa maisha na Mkuu wa shule kubakia shule hapo na atakaye tishiwa atoe taarifa kwake.
Hata hivyo Mwalimu huyo amejitetea kuwa amewarudishia fedha zao wanafunzi wote aliwachangisha, na wanafunzi nao wameuthibitishia kurudishiwa fedha zao.
.
Hivyo makala MKUU WA SHULE NA AFISA ELIMU KATA WA INGIA MATAWAN KWA KUTOZA MICHANGO WANAFUNZI
yaani makala yote MKUU WA SHULE NA AFISA ELIMU KATA WA INGIA MATAWAN KWA KUTOZA MICHANGO WANAFUNZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKUU WA SHULE NA AFISA ELIMU KATA WA INGIA MATAWAN KWA KUTOZA MICHANGO WANAFUNZI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/mkuu-wa-shule-na-afisa-elimu-kata-wa.html
0 Response to "MKUU WA SHULE NA AFISA ELIMU KATA WA INGIA MATAWAN KWA KUTOZA MICHANGO WANAFUNZI"
Post a Comment